Usitume kwa hii namba, tuma kwa ile ingine, sababu ya msemo huu yajulikana….

Usitume kwa hii namba, tuma kwa ile ingine, sababu ya msemo huu yajulikana….


This image has an empty alt attribute; its file name is CEO_PETER.png
Peter Ndegwa Afisa Mkuu wa Safaricom

Huku kampuni ya mawasiliano ya Safaricom ikitangaza faida ya shilingi bilioni 37 katika muda wa miezi sita ya mwanzo wa mwaka, imeibuka kuwa wakenya wanakopa takribani shilingi 1.34 kila siku.

Hii imepelekea wakenya kuita Kenya nchi ya Fuliza na kamari kutokana na madeni mengi ambayo nchi na wakenya kwa jumla wanadaiwa,

Wengi wametetea madeni hayo wakisema taifa na wananchi kwa jumla hawana na pesa na ndio sababu wanakopa kwa wingi.

Kwa mujibu wa Safaricom, wakenya walikopa shilingi Bilioni 242.6 kati ya Aprili na Septemba mwaka huu.

Huduma hiyo ina takribani watumiaji milioni 1.7. na iliwezesha Saaricom kupata aida ya shilingi Bilioni 2.8

Mengi ya madeni ya Fuliza ni madogo madogo na hutumika kutatua shinda ndogo ndogo za ukosefu wa fedha.

This image has an empty alt attribute; its file name is uliza-a.png

Fuliza ambayo ni huduma ya ukopeshaji inayomilikiwa na kampuni ya Safaricom na NCBA (40% kila moja) na Benki ya KCB kwa asilimia 20 na ilizinduliwa mwaka wa 2019.

This image has an empty alt attribute; its file name is uliza-aaa.png

Huduma hii huwawezesha wakenya kutuma pesa ama kulipia bidhaa ikiwa hawana pesa kwenye simu zao.

Wakenya sasa wanataka huduma hiyo idhibitiwe wakisema inanyonya pesa zao.

Hata hivyo wengine wanasema hakuna anayelazimishwa kujiunga na mfumo huo wa fuliza.

admin

Leave a Reply

Your email address will not be published.