Usicheze na fisi wa mtandaoni, tazama jinsi walivyomfilisi mrembo kwa kumuahidi ndoa

Usicheze na fisi wa mtandaoni, tazama jinsi walivyomfilisi mrembo kwa kumuahidi ndoa

Msichana mmoja mwenye umri wa miaka 25 amekwama katika eneo la Likoni kaunti ya Mombasa baada ya kugundua mpenzi wake wa mtandaoni ni laghai sugu.

Msichana huyo kwa jina Sarah anasema alisafiri kutoka mjini Nairobi akiwa na mwanaye kuja kumtembelea  mpenzi wake wa mtandaoni kwa jina Tom ambaye ni mkazi wa Likoni lakini alipofika akagundua mpenzi wake wa mtandaoni na mhusika aliyekutana naye ni vitu viwili tofauti.

Sara anasema mpenzi wake ambaye alidai kuwa ni polisi lilikuwa ni laghai lililokuwa linavizia pesa yake.

“Alipokuja nilimuuliza, ni wewe ama ni kutumwa umetumwa kwa sababu sura yako na ile ya mtandaoni ni vitu viwili tofauti.”

“Aliniambia kuwa alikua ametumwa na Tom lakini nikaogopa na nikazusha fuo watu wakaja wakanisaidia,” Sarah anasema  

Msichana huyo anasema mtu huyo kwa jina Tom alikua anatumia picha ya ofisa wa polisi tayari amefaidi zaidi ya shilingi elfu 85.

Sarah aelezea jinsi alivyokutana na mpenzi wake ghushi

“Aliniahidi ndoa na kabla ya tuoane, akaniambia nimsaidie kidogo. Si kuwa na hofu kuwa angeniruka hadi pale nilipotaka kudhibitisha mpenzi wangu ni nani”

Sarah anasema aliunganishwa na Tom na binamu yake ambaye ni mwanafunzi wa taasisi ya mafunzo ya polisi wa utawala katika eneo la Embakasi mini Nairobi.

Sara anasema amekwana Mombasa na angetaka watu hao kumrudishia pesa zake ambazo walimlaghai.

Polisi katika eneo la Likoni wameanzisha uchunguzi kuhusu kisa hicho.

Gharama ya mapenzi ghushi mtandaoni

Mapema mwaka huu idara ya Uchunguzi wa Jinai (DCI) ilionya wasichana kujipeusha na wanaume ambao wanawalaghai mitandaoni kwa kujifanya kuwa watu waliofaulu maishani.

Tume ya biashara nchini Marekani inakadiria kuwa zaidi ya dola milioni mia mbili hupotea kila mwaka kutokana na ulaghai wa mapenzi ghushi mtandaoni

Ends……

admin

Leave a Reply

Your email address will not be published.