Tuzo zote za Kiswahili zaenda Tanzania, wakenya walia ngoa

Tuzo zote za Kiswahili zaenda Tanzania, wakenya walia ngoa
Mjadala umeibuka kuhusu uandishi wa fasihi ya Kiswahili huku wakenya wakilalamika kuwa tuzo zote za Kiswahili zaenda Tanzania Kwenye mkutano wa mtandaoni ambao uliwapatia fursa washindi wa tuzo za fasihi ya Kiswahili zinazofadhiliwa na kampuni ya Mabati Rollings na Chuo Kikuu cha Cornell nchini Marekani imeibuka kuwa waandishi wa fasihi ya Kiswahili kutoka Kenya huwa hawawasilishi miswada yao. “Hili si jambo la kushtua ikizingatiwa kuwa Kiswahili ni lugha asilia ya Watanzania wengi,” akasema Walter Bgoya ambaye ni mkurugenzi mkuu wa kampuni ya uchapishaji ya Mkuki na Nyota nchini Tanzania huku akiongeza kuwa ikifikia ukwasi na matumizi ya lugha ya Kiswahili basi watanzania wanawapiku wakenya kwa msingi huo. Bgoya alisema wakenya wengi pia hushinda wakenya wengi nao hushinda tuzo za uandishi wa fasihi ya kiingereza. Tuzo za Kiswahili za Mabati Cornell hutolewa ili kuwatamabua waandishi wa fasihi ya Kiswahili ambao miswada yao  haijachapishwa. Wakfu wa msomi maarufu na mwandishi wa riwaya za Kiingereza Prof Ngugi wa Thiong’o mmoja kati ya wafadhili wa tuzo hizo. Washindi hao hupata fursa ya kuchapishwa na kampuni  ya uchapishaji vitabu za Mkuki na Nyota nchini Tanzania, na ile East African Educational Publishers nchini hapa Kenya.
Wakfu wa msomi na mwandishi wa fasihi ya Kiingereza Pro. Ngugi wa Thiong’o ni mmoja wa wafadhili wa Tuzo la fasihi ya Mabati Cornell. Picha: Kwa hisani ya Nikki Kahn/The The Washington Post kupitia Getty Images)
Kwenye mkutano wa Alhamisi washindi wa mwaka wa 2015 Anna Samwel Manyanza aliyeandika riwaya ya Penzi la Damu na Mohammed K. Ghassani aliyetuzwa kwa diwani yake ya mashairi iiitwayo  N’na Kwetu walisoma sehemu za vitabu vyao na kudhihirisha ukwasi wa lugha ya Kiswahili. Mkutano huo ulikuwa ni mmoja katika misururu ya mikutano ambapo washindi walipata fursa kusoma na kujadili tungo zao kabla ya majaji kuwatangaza waliofanikiwa kuwa kwenye orodha ya 2021.

admin

Leave a Reply

Your email address will not be published.