Tumia “vinjia vya panya” kuingia Kenya, Dr. Nyanzi amshauri Miguna

Tumia “vinjia vya panya” kuingia Kenya, Dr. Nyanzi amshauri Miguna

Msomi mbishi kutoka nchini Uganda Dr Stella Nyanzi anamshauri wakili mbishi raia wa Kenya na Canada Dr. Miguna Miguna kutumia njia za panya kusafiri hadi nchini Kenya badala ya kutumia njia za wazi ambazo zinafanya serikali kumkanyagia.

Nyanzi anasema Miguna anaweza kusafiri hadi nchini Uganda na kisha baadaye kuingia Kenya kwa njia ambayo serikali haitambua kuwa amewasili.

Miguna ambaye alikuwa awasili nchini Jumanne alikatiza safari yake mjini Berlin Ujerumani baada ya Kampuni ya ndege ya Air France kusema haiwezi kumbeba kutokana na sababu ambazo hawakuzitambulisha.

Hata hivyo Miguna alisema sababu hizo ni ilani ya serikali ambayo imekataza kampuni za ndege kumsafirisha hadi humu nchini huku akidaiwa kuwa mtu hatari.

Tutamfanyia marekebisho

Nyanzi anasema Miguna akifika nchini Uganda atafanyiwa mapambo na marekebisho ya urembo, anyolewe ndevu na kuupaka uso wake rangi, kumbandika nywele za kibrazili kumwongezea matiti na kisha kumvalisha kitenge na kumvukisha hadi nchini Kenya kwa kutumia bodaboda itakayopitia vinjia vya panya vinavyounganisha Kenya na Uganda

This image has an empty alt attribute; its file name is Miguna-a-edited.jpg
Miguna akiwa katika uwanja wa ndege mjini Berlin. Picha: Miguna Miguna

Nyanzi ambaye ni mkosoaji mkubwa wa uongozi wa Rais Yoweri Museveni wa Uganda anasema kwenye vinjia hivi kunao askari ambao hongo ndio jina lao na watampitisha Miguna kwa urahisi bora wafungiwe kilicho chao.

Nyanzi pia amesisitiza si haki kwa serikali kutumia uraia wa nchi zaidi ya moa kama silaha ya kukiuka haki za kibinadamu za mtu.

Wiki iliyopita, Miguna aliwasilisha ombi mahakamani la kutaka apatiwe idhini ya kuja nchini lakini Jaji akatupilia mbali ombo hilo kwa madai kuwa hakukuwa na ushahidi kuonyesha alikuwa amekatazwa kuingia nchini.

Miguna alifurushwa kutoka nchini Kenya muda mupi baada ya uchaguzi mkuu wa  baada ya 2017 kwa kumlisha kiapo kinara wa ODM Raila Odinga kama rais wa wananchi.

This image has an empty alt attribute; its file name is Miguna-aa.jpg
Miguna alipomwapisha Kinara wa ODM Raila Odinga

Muda mfupi baadaye Raila aliungana na Rais Uhuru Kenyatta kwa kile ambacho walikiita handisheki ambayo wanasema ilileta uwiano na maridhiano ya taifa.

admin

Leave a Reply

Your email address will not be published.