Stars yaibana Rwanda, huu ni ushindi wa simba wa sarakasi tu

Stars yaibana Rwanda, huu ni ushindi wa  simba wa sarakasi tu

Na Edwin Muthomi

Timu ya Taifa Harambee stars iliandikisha ushindi wake wa kwanza katika mechi za kufuzu kwa kombe la dunia kwa kuicharaza Rwanda mabao mawili kwa moja ugani Nyayo.

Hata hivyo ushindi huo hauna maana yoyote kwani tayari Kenya imebanduliwa kwenye kinyang’anyiro hicho huku Mali ikiibuka ya kwanza kwenye kundi E.

Huu ulikuwa ndio ushindi wa kwanza chini ya ukufunzi wake Engin Firat. Ilikuwa pia ni furaha si haba kwa kamati shikilizi baada ya FKF kutupiliwa mbali.

Engine Firat Kocha a Harambee Stars Picha; Kwa Hisani

Mshambulizi pasi Michael Olunga alitia kimiani bao la kwanza dakika ya tatu.  Olunga alikuwa msumari moto kwa kidonda chake golikipa wa Rwanda Fiacre Ntwari kwani alihusika katika mashambulizi hatari na kumfyatulia mafataki mazito.

Dakika ya kumi na tano Richard Odanda alizibusu nyavu za mgeni kupitia mkwaju wa penalty baada ya mlinda lango Fiacre Ntwari kumzuia Eric Ouma kufunga kwa njia isiyofaa.

Matokeo kwenye kundi E

Olivier Niyonzima aliwafungia Rwanda kifuta machozi dakika ya sitini na sita.

Timu ya Kenya ilimaliza kundi lao na alama sita ikiwa nambari ya tatu huku Rwanda wakishikilia mkia kwa alama moja.

Timu ya taifa Mali inaongoza kundi hilo kwa alama kumi na sita wakifuatwa na Uganda kwa alama tisa. Kenya na Rwanda wameaga kombe la dunia kwa mapema.

admin

Leave a Reply

Your email address will not be published.