Stars kumenyana na Rwanda Jumatatu, mashabiki hawana matumaini

Stars kumenyana na Rwanda Jumatatu, mashabiki hawana matumaini

Matokeo duni yamezidi kuisonga timu ya Harambee stars huku ushiriki wa michuano mikubwa ikibaki ni ndoto tu.

Matokeo hayo yametiliwa cheche na migogoro ya uongozi na madai ya ufisadi ambayo yanakabili timu hiyo huku makocha wake wakibadilishwa kama tambara mbovu.

Stars imekuwa ikiandikisha matokeo mabovu na hata wakati mmoja kulimwa mabao matano bila jibu na Mali.

Walitoka sare mkondo wa kwanza na wa pili na timu ya Uganda na leo wanatazamiwa kukabiliana na Rwanda zote zikiwa ni mechi za kufuzu kwa kombe la dunia mwakani.

Kwa mujibu wa Odongo Odhiambo, FKF inafaa kuwakagua makocha inaowatafuta. “Mara nyingine wanaleta makocha ambao hawaelewi soka ya Kenya. Makocha wengine wanawatoa wachezaji wenye uzoefu na kuwaleta wageni”

Uongozi mbaya unaharibu soka

Swala la wachezaji na maslahi kushughulikiwa limekuwa katika vinywa vya  wengi pamoja na mashabiki wanaoisapoti Harambee stars.

Evans Mwirigi anafafanua, “Nadhani kuna ufisadi kwa sababu wakati mwengine fedha za wachezaji hazijakuwa zikitoka na wanateseka mahotelini. Jingine ni kwamba kuna ukabila. Kikosi cha juzi wachezaji wengi walitoka timu chache. Wanafaa kuangalia talanta nzuri kote kote nchini.”

Viwango vya Mashabiki pia ni changamoto hapa nchini kulingana na baadhi ya Mashabiki.

Arman Kipruto mtangazaji na mpenzi wa soka anasema. “Tuko na tatizo katika niwango vya wachezaji wetu. Hivi majuzi bao alilofungwa mlinda lango Brian Bwire lilikua la makusudi kwa faida ya Uganda.”

Uwajibikaji na jambo muhimu sana katika soka na usimamizi wake, ukikosekana basi soka itadhoofika.

Abdul Komora shabiki wa Harambee alichangia, “shida ya Harambee stars na soka nchini ni uongozi. Baadhi ya viongozi hawawajibikii majukumu yao na hivi unapata  soka yetu inadidimia kimatokeo. Baadhi pia ya wachezaji wa Harambee stars hawajafikia kiwango cha kucheza soka ya kimataifa na hivyo hawatoki na ushindi”

Ufadhili wa kutosha

“Soka hapa nchini haipati ufadhili wa kutosha. Unapata kwamba mara nyingi wachezaji wakienda kucheza mechi za kimataifa wanatatizika kimalazi. Serikali imafaa kutia soka kipau mbele” anasema  Mercy Njeri shabiki sugu wa soka.

Ni bayana kwamba dondadugu la uongozi mbaya umeadhiri sana soka nchini Kenya. Kwa sasa rais wa Shirikisho la Soka nchini Nick Mwendwa anakabiliwa na tuhuma za ufisadi na anahojiwa na makachero wa DCI.

Waziri wa michezo na utamaduni Amb. Amina Mohammed alilibandua shirikisho la soka FKF kutokana na madai ya ufisadi. Aliteua kamati shikilizi inayoongozwa na Jaji mstaafu Aaron Ringera.

admin

Leave a Reply

Your email address will not be published.