Serikali saidia… Wanubi walia kutelekezwa na serikali..

Serikali saidia… Wanubi walia kutelekezwa na serikali..

 Na Victor Moturi

Wanubi wanaoishi Kibera wanahangaika kwa kukosa kutambuliwa kama wakenya licha ya kuwa wameishi humu nchini kwa zaidi ya miaka mia moja sasa.

Mababu za Wanubi hao waliletwa na wakoloni humu nchini katika mwanzo wa miaka ya 1900 kama walinzi na askari wa wakoloni hao.

Hata hivyo vizazi vya sasa vinadai havina kwao kwani serikali ya Kenya haiwatambui, Waingereza walirudi kwao na wala hawezi enda Sudan ambako ndio kitovu chao.

Kwa mujibu ya baadhi ya vitukuu vya Wanubi hao, baadhi yao hawawezi pata vitambulisho, ajira na hata kupiga kura kwa vile hawana vyeti muhimu kama vile kadi za kuzaliwa.

Afisi za shirika linalotetea haki za WAnubi katika eneo la Kibra, mjini Nairobi

Ashiff Obwaka mwenye umri wa miaka 23 anasema amengoja kitambulisho chake kwa muda wa miaka miwili sasa.

“Sina kazi na maisha yamekuwa magumu. Tumeitwa mikutano, tumeenda vetting lakini sijapata kitambulisho. Pia tungetaka kupiga kura kama wakenya wengine lakini nani atakuandikisha bila kitambulisho?,”  Ambaka aneelzea masaibu wanayopata.

Anasema pia hawezi fungua hata account ya bank na hata akiwa mgonjwa hawezi tibiwa kama mwananchi kwani hana bima ya NHIF.

Ukosefu  wa hati muhimu umechangia kwa wanubi hao kukosa kujiendeza kielimu hasa wanapofikia ngazi muhimu kama vile elimu ya chuo kikuu.

“Hatuwezi kupata ufadhili wa elimu kutoka kwa hazina ya ufadhili wa elimu ya juu HELB na wazazi wetu wanang’ang’ana kweli” anasema Abdul Said Shaban ambaye ni mwanafunzi katika chuo kikuu cha kibinafsi cha Daystar

Wanubi hawa hupitia masaibu wanapotaka kupata vitambulisho kwani lazima wakaguliwe sana na hili huwachukua muda mrefu sana.

Mmoja wa wazee wa kijiji Mzee Babala anasema wanapeleka majina kumi ya wale ambao wanataka kupata vitambulisho kwa wakati mmoja.

“Tukishafikisha watoto kumi unaitisha grassroot vetting  committee ya hapa Kijijini mnaanza kukagua hawa watoto ni akina nani. Kisha hiyo orodha unapelekea chifu. Kisha chifu atapanga na registrar officer, sasa watapanga tarehe yenye tutaenda vetting. Hatujui ni nini maana kila mahitaji wanataka tunawapea inaenda Nairobi inakaa, tukiuliza tunaambiwa bado kuna uchunguzi tunafanya ama taaria za baadhi ya watoto hazilingani.”

Serikali ya Kenya iliwachukulia Wanubi kama mzigo wa waingereza kwani wao ndio waliowaleta humu nchini.

Kwa mujibu wa mashirika yasiyo ya kiserikali, ukosefu wa hati muhimu umewakosesha Wanubi nafasi ya kushiriki katika uongozi na mendeleo jambo ambalo kulingana na mshirikishi wa vuguvugu la haki za wanubi, Shay Hussein ni ukiukaki mkubwa wa haki za kibinadamu.

“Niliandikia bunge lakini katibu wa bunge alisema tayari tumewasilisha keshi mahakamani na kwa hivyo bunge haliwezi kutushughulikia. Hata hivyo nimezungumza na mwakilishi wa eneo letu Imran Okoth ambaye analifuatilia swaala hili.” Anasema Hussein.

Kwa sasa waziri wa usalama wa ndani Dr. Fred Matiang’i amepewa siku 90 kuweka mikakati ya kuwashughulia Wanubi na kuwatambua kama wakenya.

Victor Moturi ni mwandishi mahiri kutoka mjini Nairobi ambaye ameshinda tuzo kadhaa kutokana na taarifa anazoandika kuhusu afya na kilimo katika eneo la Afrika Mashariki

admin

Leave a Reply

Your email address will not be published.