Ruto apigwa mawe Kisumu, demokrasia yaomboleza…

Ruto apigwa mawe Kisumu, demokrasia yaomboleza…

Msafara wa naibu wa rais William Ruto umepigwa mawe mjini Kisumu na kupekekea mvutano kati ya wanaomuunga mkokoni na wale wanaompinga.

Ruto alikuwa anahutubia mkutano katika eneo la Kondele pale vurugu lilipoanza na kupelekea kurushwa kwa mawe yaliyoharibu magari kadhaa.

This image has an empty alt attribute; its file name is 254916886_10228147723626726_1610499337764202146_n.jpg
Mojawapo wa magari yaliyoharibiwa Kisumu

Yasemekana watu hao wanaoaminika kuwa wafuasi wa chama cha ODM walimzoma Ruto huku wakimwambia kuwa wanataka elfu sita zinazoahidiwa na kinara wa ODM Raila Odinga kama njia ya kumkaba Ruto kwenye mfumo wake wa wilbaro.

Ilibidi Ruto kukatisha mkutano wake na kuondolewa na polisi mahali hapo na kuelekea Migori.

Kwa mujibu wa polisi, Ruto anafaa kulaumiwa kwani tayari alikuwa amefahamishwa kuwa kuna mivutano kuhusu fedha za kupanga mikutano.

Msemaji wa polisi Bruno Shioso anasema tayari upande wa Naibu wa Rais ulikuwa umefahamishwa kuhusu mivutano hiyo lakini ukakadi

Shioso hata hivyo amesema kuwa Ruto aliondolewa mahali hapo akiwa salama na hakuna mtu aliyeumia.

This image has an empty alt attribute; its file name is police.jpg
Taaria ya polisi kuhusu vurugu la Kisumu, Ruto anafaa kulaumiwaLakini kwa mujibu wa baadhi ya wapinzani wa Ruto huenda upande wake ulipanga njama ya kumpiga mawe.

Kulingana na wakili wa Nairobi, Wahome Thuku, Ruto alipanga njama hiyo ili kuepuka kuwalipa watu pesa alizoahidi.

Thuku ni mfuasi sugu wa Rais Uhuru Kenyatta na anampigia debe kinara wa ODM Raila Odinga kumridhi Rais Kenyatta atakapostaafu mwishoni mwa mwaka ujao.

This image has an empty alt attribute; its file name is wahome.png
Thuku anadai Ruto alipanga njama ya kumpiga mawe


Hata hivyo kwa mujibu wa mmoja wa maafisa wa mawasiliano wa Ruto Dennis Itumbi njama hiyo ilipangwa na wafuasi wa chama cha ODM.


Madai ya Itumbi. ODM ilipanga njama kumfurusha Ruto

admin

Leave a Reply

Your email address will not be published.