Mwendwa apaaza sauti, soli Amina, niko kwenye usukani

Mwendwa apaaza sauti, soli Amina, niko kwenye usukani
Waziri wa Michezo BAlozi Amina Mohamed

Rais wa shirikisho la kandanda nchini Nick Mwendwa amepinga hatua ya waziri wa michezo Amina Mohamed kumlisha kandi nyekundu na kubandua shirikisho analoongoza.

Balozi Amina alhamisi asubuhi alicheza ngware na kulivunja shirikisho hilo huku akimchagua Jaji mstaafu Aaron Ringera kama mwenyekiti wa kamati shikilizi.

Ringera atakukumbukwa kwa kuongoza kikosi cha “Radical Surgery” ambacho kiliteuliwa na Rais Mwai Kibaki muda mfupi baada ya kuchaguliwa mwaka wa 2003.

Kikosi hiki kiliwafuta majaji wengi kazi kufuatia madai ya ufisadi ingawa wengine walidai ilikuwa fursa ya kulipiza kisasi.

Amina alichukua hatua ya kumlisha Mwendwa kadi nyekundu kufuatia ripoti ya msajili ya michezo aliyependekea kuvunjwa shirikisho hilo kwa madai kuwa Mwendwa na wenzake walikuwa wanachezea fedha kinyume na kanuni.

Amina na Mwendwa wamekuwa wakivutana kwa muda kuhusu matumizi ya fedha ambazo serikali inalipatia shirikisho hilo.

Mwendwa kwa upande wake amepinga hatua ya kumtimua akisema yeye bado ni rais wa shirikisho.

Kwenye mkutano na waandishi wa habari Mwendwa amesisistiza kuwa Shirikisho hilo si idara ya serikali na haliwajibiki kwa waziri wa michezo.

Ameongeza kuwa shirikisho hilo huzingatia kanuni za FIFA na hatua ya kumbandua yeye na kamati yake ni kama kupiga penalti ya kombo.

Mwendwa na kamati yake wanadaiwa kufuja takribani shilingi milioni 430 zikiwa ni malimbikizi ya pesa walizopewa na serikali kushiriki michezo ya kanda na bara.

This image has an empty alt attribute; its file name is Ca2Iq42WcAES6h8.jpg
Sam Nyamweya, mmoja wa wapinzani sugu wa Mwendwa amefurahia hatua ya waziri Amina. Picha: Kwa Hisani

Wapinzani wa Mwendwa wakiwemo Sam Nyamweya wamesherekea kutolewa kwa Mwendwa wakisema hatua hiyo itasaidia kuimarisha soka nchini.

Nyamweya na baadhi ya washirika wake walisusia uchaguzi wa FKF huku wakimshtaki Mwendwa kwenye mahakama ya migogoro ya michezo ambapo walipoteza kesi zote.


admin

2 thoughts on “Mwendwa apaaza sauti, soli Amina, niko kwenye usukani

Leave a Reply

Your email address will not be published.