Mwendwa aonjeshwa kamata kamata Friday, ajua si mpendwa…..

Mwendwa aonjeshwa kamata kamata Friday, ajua si mpendwa…..

Na Edwin Muthomi

Masaibu ya Rais wa Shirikisho la soka nchini Nick Mwendwa yanazidi kuongezeka huku Mwendwa akihojiwa na idara ya upelelezi kuhusiana na madai ya ufisadi katika Shirikisho la Soka nchini FKF.

Mwendwa alikamatwa na maafisa wa DCI katika hoteli moja eneo la Westlands alipokuwa anakutana na wachezaji wa Harambee stars walipokuwa wanajadili mechi ya Stars ya Jumatatu ijayo dhidi ya Rwanda.

Mwendwa na timu yake walibanduliwa alhamisi na waziri wa michezo Amina Mohamed kwa madai ya kuchezea fedha za Shirikisho ngware chafu.

Hatua hiyo ilipingwa na Mwendwa ambaye pia aliungwa mkono na Shirikisho la Soka Ulimwenguni FIFA.
FIFA kwenye barua ilionya itachukulia serikali hatua na kupiga marufuku timu za Kenya kushiriki katika michezo ya kimataifa.

Ringera aanza kazi

This image has an empty alt attribute; its file name is ringera.jpg
Jaji Mstaafu Aaron Ringera PIcha: Wakfu wa Jaji Ringera

Hayo yamejiri huku kamati ya muda ya soka ikisimamisha ligi zote kwa wiki mbili kuanza tarehe kumi na mbili mwezi huu.

Kamati hiyo inayoongozwa na Jaji mstaafu Aaron Ringera imedokeza kupitia taarifa kwa vyombo vya habari kwamba watakuwa wakizungumza na washikadau, vilabu pamoja na wachezaji ndiposa kuboresha kiwango cha soka.

Ligi hizo ni ikiwemo ligi kuu ya FKF kwa wanaume na wanawake, ligi ya Kitaifa na ligi ya daraja la kwanza wanaume na wanawake.

Ligi zinazocheza katika branchi na pia branchi ndogo zitakuwa zikiendelea kama kawaida. Wanakamati wamewahakikishia wakenya kwamba shughuli za soka nchini na nje zitaendeshwa vyema.

Ligi hizi zinatarajiwa kurejea tarehe ishirini na sita mwezi huu.
Uamuzi huu umetokea siku moja baada ya Waziri wa mchezo Amina Mohammed kulivunja shirikisho la soka nchini Kenya FKF na usimamizi wake.

admin

One thought on “Mwendwa aonjeshwa kamata kamata Friday, ajua si mpendwa…..

Leave a Reply

Your email address will not be published.