Mwanafunzi darasani, fundi mjengoni, fahamu jinsi wanafunzi wa vyuo wanavyokabili maisha.

Mwanafunzi darasani, fundi mjengoni, fahamu jinsi wanafunzi wa vyuo wanavyokabili maisha.

Na Edwin MUthomi

This image has an empty alt attribute; its file name is roti-5599559_960_720.jpg
Chapati ni chakula kinachoenziwa na wanafunzi

Mwandishi wa tamthilia marehemu Francis Imbuga aliandika kwamba wanafunzi wana pesa akilini, ila ndoto zao zitawafikisha mbali.

Ila lengo la kufanikisha ndoto hizo ni kazi, kuna changamoto si haba na wanafunzi hasa kutoka familia zisizo na uwezo mkubwa wa kifedha hung’ang’ana si haba.

Kwa baadhi ya wanafunzi katika Chuo cha Mafunzo Anuai cha Pwani (KNCP) ambao wanajitegemea kifedha, kupiga mbizi katika bahari hii lazima uwe na moyo, bidii na ndoto dhabiti.

Daniel Mbindi mwanafunzi wa mwaka wa kwanza, “Mimi hupokea fedha kutoka kwa wazazi pekee, natumia shilingi kumi ama ishirini kwa siku. Hii ni kwa sababu nina unga na mafuta na bei ya mboga ni shilingi kumi.”

“Tunagawa matumizi. Twanunua mboga peke yake. Mchana naweza kosa chamcha sababu mimi hula chakula kilicho lala asubuhi. Tatizo ni kuwa hatupati ile lishe bora. Kando na hilo nina chaneli ya YouTube ambayo inanipa kitu kidogo.”

Wahenga wamenena kuwa ukikosa la mama hata la mbwa huamwa. Kwake Brian Otieno kukosa pesa za kutosha kunamfanya achangamke.

“Huwa natumia kama themanini kwa siku. Asubuhi natumia ishirini kwa chai, mchana napata kuchomewa chapati tatu. Wakati mwingine naenda kibarua kama kwa mjengo na napata pesa.

Ni bayana kwamba kuna tofauti ya matabaka chuoni kwani baadhi ya wanafunzi wanatumia pesa zaidi.

Matabaka chuoni


Ida Loyo anasema hutumia takribani mia tano kwa siku. “Mimi hutumia mia tatu kwa usafiri na chamcha na kutenga kati ya mia moja hadi mia moja hamsini ya chajio.”

Anadokeza kuwa yeye hupata ufadhili kutoka kwa wazazi, dadake na pia shangazi. Ili kijikimu binafsi, anadhamiria kufanya biashara ya kuchuuza mitumba shuleni wakati wa mapumziko.

Sharon Awuor anasema hujituma na kuuza pipi pamoja na biskuti shuleni.

“Naweza napata faida ya mia tatu kila siku. Hizi pesa hazitoshi kunifadhili kwa sababu biashara ina changamoto zake. Napata fedha za matumizi pia kutoka kwa walezi wangu. Nikimaliza pia nataka kuanza biashara kubwa kuliko hii”

Ann Ouma ambaye amekamilisha masomo yake kozi ya uhasibu anawapa moyo wenzake.

Anawasihi kwamba changamoto ni nyingi na lazima wazipange fedha zao vilivyo pamoja na kuwa wabunifu katika biashara zao. “Unaweza ukashuhulikia biashara mpaka ukasahau masomo, na ukifeli masomoni utakuwa hujatimiza lengo lako”.

Anakamilisha kwamba kusoma na kumaliza ni kwa neema ya mwenyezi Mungu.

Baadhi ya wanafunzi hutegemea ufadhili wa wazazi, na washikadau mbali mbali katika elimu kwa mfano bodi ya ufadhili wa elimu ya juu ili kuwawezesha kusoma kwa utulivu na amani.

admin

Leave a Reply

Your email address will not be published.