Muwaniaji wa MCA Utawala afariki ajalini

Muwaniaji wa MCA Utawala afariki ajalini

Mmoja wa wawaniaji wa uwakilishi wadi katika eneo la Utawala mjini Nairobi ameaga dunia.

Mike Mwathi Gitonga alifariki katika eneo la Afro Sayari kwenye barabara ya Eastern by-pass inayounganisha eneo la Ruiru na uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta.

Marehemu Mike Mwathi Gitonga

Gitonga alikuwa anawania kiti hicho cha uwakilishi wadi kupitia chama cha New Democrats.

Yasemekana Gitonga mwenye umri wa miaka 43 ambaye pia alikuwa mfanya amemuacha mjane na mtoto mmoja.

admin

Leave a Reply

Your email address will not be published.