Moses Kuria kumenyama na Ruto katika uchaguzi wa uwakilishi wadi wa Kiagu, Meru

Moses Kuria kumenyama na Ruto katika uchaguzi wa uwakilishi wadi wa Kiagu, Meru

Hatimaye Moses Kuria ambaye yuko hospitalini ana sababu ya kutabasamu baada ya mahakama kuu kuamua kuwa muwaniaji wa chama chake atashiriki kwenye uchaguzi mdogo wa eneo la uwakilishi wadi la Kiagu Kaunti ya Meru

Militon Mwenda wa Chama cha Kazi alikuwa amepigwa kalamu ya kutoshiriki uchaguzi kutokana na kile kilichodaiwa ni kukosa kujiuzulu kutoka kwa uajiri wa umma.

Kutokana na hatua hiyo Tume ya Uchaguzi ilitoa ilani ya masaa sabini na mawili kwa Chama cha Kazi kinachoongozwa na Kuria kuteua mgombea mwingine

Hata hivyo muwaniaji huyo na mwenzake Nathan Gitonga wa chama National Ordinary People Empowerment Union-NOPEU walienda mahakamani na kupinga marufuku hiyo

Mahakama kuu iliamua kuwa wawili hao wanaweza kushiriki uchaguzi huo ambao sasa utafanyika tarehe 16 Disemba

This image has an empty alt attribute; its file name is 25e852a413.jpg
Wafula Chebukati Mwenyekiti IEBC PIcha: Kwa HisaniKwenye arifa mwenyekiti wa tume hiyo Wafula Chebukati amesema kampeini zitafanyika kati ya Novemba tarehe moja hadi Disemba tarehe 13.

This image has an empty alt attribute; its file name is Capture.png


Uchaguzi huo utatoa fursa kwa waliokua wendani wa kisiasa kupimana nguvu huku Kuria akimkabili muwaniaji wa mshirika wake wa zamani Wiliam Ruto wa chama cha UDA.

Uchaguzi huo uliokuwa ufanyike tarehe 16 Oktoba unatokana na kifo cha marehemu Eunice Karegi aliyekuwa mmoja wa waakilishi wadi wa kike wawili waliochaguliwa katika kaunti ya Meru.

admin

Leave a Reply

Your email address will not be published.