Mlipuko mwingine watokea Uganda, watu wawili wafariki

Mlipuko mwingine watokea Uganda, watu wawili wafariki

Watu wawili wamefariki na kufikisha idadi ya watu waliofariki kutokana na visa viwili tofauti vya milipuko ya mabomu nchini Uganda kufikia watatu.


Kisa cha pili kilitokea mwendo wa saa kumi na moja jioni katika wilaya ya Mpigi katika barabara ya Kampala kwenda Masaka.

Kwa mujibu wa Rais Museveni mlipuko huo ulitokea baada ya bomu lililokuwa limetegwa kwenya basi kulipuka na kuwaua watu wawili na kuwajeruhi wengine.

This image has an empty alt attribute; its file name is Museveni.png

Yasemekana basi hilo lilikuwa linasafiri kutoka Kampala kwenda Bushenyi na umetokea siku mbili baada ya mlipuko mwingine uliomuua mhudumu mmoja wa hoteli mnamo siku ya Jumamosi.

Haikufahamika mara moja milipuko hii ilipangwa na nani ingawa katika mlipuko wa Jumamosi kwenye eneo moja la burudani mjini Kampala kundi la kigaidi la Islamic State lilikiri kuhusika.

This image has an empty alt attribute; its file name is Museveni-aaa.png

Rais Yoweri Museveni amesema kuwa serikali yake itawawawinda magaidi hao na kuhakikisha waliojeruhiwa wamepata haki.

This image has an empty alt attribute; its file name is museveni-aa.png

Tayari serikali ya Uingereza ilikuwa imetoa tahadhari kuhusiana na uwezekano wa kutokea mashambulizi ya kigaidi huku ikiwaonya raia wake kuhusu kusafiri hadi nchini humo .

Milipuko hiyo inakumbusha kuhusu shambulizi la mwaka wa 2010 ambapo raia 74 wa Uganda waliuawa wakati magaidi waliposhambulia mashambiki wa soka waliokuwa wanatazama fainali za kombe la dunia katika uwanja wa raga mjini Kampala

admin

Leave a Reply

Your email address will not be published.