Mgombea useneta Mombasa Hamisi Mwaguya adadia wilbaro, Mombasa kuna nini?

Mgombea useneta Mombasa Hamisi Mwaguya adadia wilbaro, Mombasa kuna nini?

Mgombea wa kiti cha useneta kaunti ya Mombasa Hamisi Mwaguya ametangaza kuhamia chama cha UDA kinachoongozwa na Naibu wa Rais William ruto

Mwaguya ametangaza hilo kwenye ukurasa wake wa Facebook ambapo amesema kuwa amevutiwa na sera ya naibu wa rais ya kuanzia chini kwenda juu maarufu kama “wilbaro.”

This image has an empty alt attribute; its file name is Capture-1.png

Mwaguya amehamia UDA siku chache baada ya binamu yake gavana wa Mombasa Amir Joho kuhamia chama hicho cha UDA.

Ingawa baadhi ya watu wameikashifu hatua hiyo, kuna wengine waliomteteta wakisema kuwa Hamisi amefungiwa milango katika chama cha ODM ambacho kinasemekana kuwa na umaarufu mwingi katika kaunti ya Mombasa

Hata hivyo kuhama kwa Mwaguya ni ishara kuwa penye moshi pana moto na chama cha ODM kimeendelea kupoteza umaarufu wake pwani.

Kwa mfano mwishoni wa wiki iliyopita kinara wa ODM Raila Odinga alikuwa Pwani ambapo baadhi ya wanasiasa wakiwemo magavana hawakutia guu kwenye mkutano wake.

Gavana Amasson Kingi wa Kilifi na Hassan Joho wa Mombasa hawakuwa kwenye msafara wa Raila.

Kingi ameanzisha chama chake cha Pamoja African Alliance (PAA) ambacho kimeiteka nyara kaunti ya Kilifi kiasi ambacho kwa sasa haisikii la mwadhini wala mteka mai msikitini.

Kwa upande wake Gavana wa Mombasa Hassan Joho ambaye pia ni naibu kiongozi wa chama cha ODM alisemekana kuwa nje ya nchi kwa hivyo hangewaandamana na Baba.

Ingawa hivyo kuhama kwa washirika wake wa karibu kutoka ODM kunapelekea kuwepo kwa maswali mengi ambayo kufikia sasa hayana jibu.

admin

Leave a Reply

Your email address will not be published.