Mechi za kufuzu kombe la Dunia zaendelea, Kenya kubakia mpenzi mtazamaji

Mechi za kufuzu kombe la Dunia zaendelea, Kenya kubakia mpenzi mtazamaji
This image has an empty alt attribute; its file name is world-cup-878463_960_720.jpg

Na Edwin Muthomi

Michuano ya kufuzu kwa kombe la dunia katika bara la Afrika itakuwa ikiendelea leo huku timu kadhaa zikishuka uwanjani kumaliza udhia. Mashindano haya yataandaliwa nchini Qatar Disemba mwakani.

Wanafarao Misri wakiongozwa naye mshambulizi matata wa Liverpool Mohammed Salah ndio wa kwanza kutia guu ndani baada ya kutoka sare ya mawili kwa mawili na Angola.

Kwinginkeko wanachipolopolo Zambia watakuwa wakifufua matumaini yao ya kufuzu huku wakimkaribisha Mauritania ugani National heroes kuanzia saa kumi.

Timu ya Zambia inajivunia wachezaji madhubuti, baadhi yao wakisakata kandanda ya kulipwa ligi kuu nchini Uingereza.

Wachezaji hao ni Patson Daka Mshambulizi wa Leicester City, Kiungo wa Brighton and Holve Albion Enock Mwepu aliyebandikwa ‘computer’ pamoja na beki wa Rangers ya uskoti Fashion Sakala.

Zambia na Mauritania wananing’inia nafasi ya tatu na ya nne mtawalia.

Tunisia wanaliongoza kundi hilo wakifuatwa na Equatorial Guinea. Wababe hawa watakuwa wakituana ugani Nuevo Estadio de Malabo kuanzia saa moja usiku. Tunisia wana uwezo mkubwa wa kufuzu.

Isitoshe baada ya kumwita Odion Ighalo kwenye kikosi chao, Super Eagles wa Nigeria watakuwa ugenini dhidi ya Liberia ugani Grande stade de Tanger saa moja jioni.

Mechi ya kwanza Nigeria walimlaza mabao mawili kwa beufe. Kocha wa Nigeria Gernot Rohr alinukuliwa akisema kuwa kikosi chake kinaenda vizuri. “Tulikuwa na wakati mzuri wa mazoezi, tumefanya mazoezi ya kufyatua mashoti na wachezaji wako sawa. Hapa Morroco hali shwari. Tunapiga jaramba kujitayarisha kwa mechi.”

Mshambulizi pasi wa Napoli Victor Osimhen yuko katika kikosi hicho. Nigeria wanaongoza huku Liberia wakikamatilia mkia.

admin

Leave a Reply

Your email address will not be published.