Mabadiliko ya tabia nchi yatisha, nchi wanachama kukutana Scotland kujadili mwelekeo

Mabadiliko ya tabia nchi yatisha, nchi wanachama kukutana Scotland kujadili mwelekeo

Katika muda wa wiki mbili zijazo wakuu wa serikali na nchi watakutana Glasgow nchini Scotland kwa kongamano la nchi washirika wa mazingira kujadili jinsi ya kukabili mabadiliko ya tabia nchi.
Kongamano hilo linatarajiwa kuleta pamoja nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa na litafanyika kuanzia 31 Oktoba hadi Novemba 12 mwaka huu.
Kongamano linafanyika kwa ushirikiano kati Uingereza na Italia na linaonekana kama hatua ya mwisho katika juhudi za kukabili mabadiliko ya tabia nchi ambayo yameonekana kuleta madhara makubwa katika mazingira na maisha ya binadamu kwa jumla.

This image has an empty alt attribute; its file name is OGB_120302_Bangladesh_Champa-stands-in-damaged-house-1024x682.jpg
Athari za mafuriko nchini Bangladesh Picha: Kwa hisani ya Oxfam

Kwa sasa ulimwengu umegubikwa na hofu ya mabadiliko ya hali ya anga ambayo yamesababisha baa la njaa, kupanda kwa viwango  vya joto, kuyeyuka kwa barafu katika sehemu zenye baridi, kuongezeka majanga kama vile mafuriko, joto na ukosefu wa mvua na baa la njaa, ongezeko la idadi ya watu wanaofariki, ongezeko la hewa chafu, kufariki na kuangamia kwa wanyama walio wachache na kupanda kwa viwango vya maji baharini.

Mafanikio ya COP-21

Kongamano hilo pia litafuatilia mafanikio yaliyopatikana tangu kongamano la mwaka 2015 mjini Paris Ufaransa ambalo linajulikana COP-15 na ambalo mataifa 196 yalikubaliana kupunguza viwango vya gesi chafu kwenye mazingira kama nia ya kukabili viwango vya joto.
Kwenye kongamano hili macho yataelekezwa kwenye mataifa ambayo yanachangia katika uchaguzi wa mazingira. Kulingana na Shirika la Kawi ulimwenguni mataifa matano yakiwemo China, Marekani, India, Jumuia ya Urusi, na Japan ndiyo yanayotoa viwango vya juu zaidi vya gesi chafu.
Baadhi ya viongozi wa nchi hizo zenye kulaumiwa kwa uchafuzi wa hewa na kuchangia mabadiliko ya tabia nchi huenda hawatahudhuria kongamano hilo.

Wachafuzi wa mazingira


Baadhi yao ni Pamoja na rais wa Uchina Xi Jinping, Rais wa Urusi Vladmir Putin na Rais wa Brazil Jair Bolsonaro.
Pia Malkia Elizabeth wa Uingereza na Kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Francis hawatahuhudhuria kongamano hilo. Kwa mujibu Shirika la Kawi, mabadiliko ya tabia nchi yanasababishwa na mambo kama vile, kuchoma mkaa, mafuta na gesi ambazo zinatoa hewa ya aina ya carbon na ile ya nitrogen, kukata miti na kupunguza misitu ambayo husaidia katika kusafisha hewa, ongezeko la ufugaji wa wanyama ambao hutoa hewa aina ya methane wanapotafuna chakula chao, kilimo kinachotumia mbolea aina ya nitrogen ambayo hutoa hewa chafu ya nitrogen oxide na gesi zinazotokana na mashini na bidhaa ambazo hutoa hutoa hwa chafu za fluorine.

Ongezeko la joto


 Kulingana na Jumuia ya Nchi za Ulaya kipindi cha mwaka wa 2011-2020 kilikuwa ni chenye joto jingi zaidi huku joto likipanda kwa zaidi ya asilimia 1.1%. Kwa sasa inakadiriwa kuwa joto linaongezeka kwa kiwango cha 0.2% kila mwaka.

admin

Leave a Reply

Your email address will not be published.