Liverpool yainyonga Man United, Mashabiki waingia mitini kuficha aibu

Liverpool yainyonga Man United, Mashabiki waingia mitini kuficha aibu

Liverpool iliiipokeza Manchester United adhabu ya kipigo cha mbwa koko msikitini na kuwaacha mashabilki wake hoi wasiwe na la kusema

Mechi hiyo iliyochezewa uwanjani Old Trafford imeona Liverpool ikiipiiga United mabao matano bila jibu katika kile ambacho mashabiki wa Manchester wamesema ni aibu isiyo kifani.

Kiungo muhimu wa United Paul Pogba alilishwa kadi nyekundi na kuoongezea masaibu ya Manchester mbele ya mashabiki wa nyumbani.

Masaibu ya Man Unted yalianza kunako dakika ya tano pale Naby Keita alipofunga bao la kwanza naye Diogo Jota akaongeza lingine kunako dakika ya 13.

Mohamed Salah alifunga midomo ya mashabiki na kuzamisha matumaini ya vijana wa Ole Gunnar Solskjaer pale alipofunga mabao matatu katika dakika ya 38, muda wa ziada wa dakika ya 45+5 na ile ya 50.

Kichapo hicho aidha kitaongezea shinikizo la kumtaka kocha Ole Gunnar ang’atuke mamlakani kutokana adhabu ambayo imekuwa ikipata katika muda wa hivi karibuni

Mabao hayo yalizamisha na kulipia kimya cha mashabiki. Tazama walivyofanya


Shabiki sugu wa Man United Eric Gates Mgenge alisema Jumatatu atakuwa katika kituo cha polisi cha Bamburi mjini Mombasa kuweka usafi kama alivyoahidi ikiwa Liverpool ingeishinda Man U

admin

Leave a Reply

Your email address will not be published.