Kutana na mwana aliyekataliwa aliyegeuka mtetezi wa haki za kijinsia

Kutana na mwana aliyekataliwa aliyegeuka mtetezi wa haki za kijinsia


Tabasamu safi kwenye uso mwororo na unaoficha umri wake inasema kuwa mhusika anayo kila sababu ya kusherehekea maisha na uhai wake.

Hata hivyo Francis Odee Omari ameyashuhudia yote na kicheko kingi, kelele na hata kuingiliana na watu kwa urahisi inaficha uchungu wa kumpoteza mamake akiwa mchanga kutokana na tamaduni zilizopitwa na wakati.

Odee anasema kuwa mamake aliuawa kwa sababu ya kuwazaa vijana mapacha na kulingana na tamaduni za wa Maragoli hiyo haikuashiria bahati nzuri kwenye familia.

Kwa hivyo ilikuwa ni aidha mimi na ndugu yangu tufe ama mama yetu auawe.

Hata hivyo Odee anasema babake alipinga wazo hilo lakini familia ilishikilia kuwa bahati hiyo mbaya ingeondolewa.

Odee anasema kuwa kwa mujibu wa shangazi yake mamake aliyekuwa wa asili ya Tanzania alinyeshwa sumu na kufariki huku ikibidi babake awatoroshe kutoka nyumbani ili kunusuru maisha yao.

Mkimbizi hadi Tanzania

Babangu alikimbilia Tanzania ambako tulikulia kwa muda.

Nilipofahamu jinsi mamangu alivyofariki niliapa kuwa sitakubalia kuona mwanamke mwingine akiteseka kutokana na tamaduni potovu, Odee ambaye hivi karibuni ametawazwa kama mwanahabari mshirika wa karibu wa maswala ya kijinsia anasema

Tangu hapo mwandishi huyu aliyesomea chuo cha mafunzo ya mawasiliano cha KIMC amekuwa akiandika na kufanya taarifa ambazo zinatetea maswala ya wanawake na wasichana waliodhululumiwa.

“Mara nyingi wanawake na wasichana hudhulumimwa na kukandamizwa na tamaduni za zamani na kuna haja ya mtu kusimamama na kuwatetea lau sivyo maisha yao yatakuwa ya taabu sana,” Odee anasema.

Kuokoa maisha ya msichana

This image has an empty alt attribute; its file name is odee-aaaa-1.jpg
Odee na mpiga picha wake walipofuatilia habari za msichana aliyetekwa nyara na kupelekwa Tanzania

Kazi yake ya kuandika taarifa za kina mama waliodhululumiwa imemfanya kusafiri katika pembe zote za nchi na hata katika eneo la Afrika Mashariki akifuatilia kufichua dhuluma hizo.

“Wakati mmoja niliandika taarifa ya mwanamke ambaye alikuwa anaishi maisha ya uchochole katika eneo la Mathare humu mjini Nairobi ambapo serikali ya kaunti ya Nairobi iliingilia kati na kujaribu kuimarisha maisha yake,” Odee anaelezea huku akiongezea kuwa mama huyo alichukuliwa na hata kupelekwa kwenye makao ya kubadilisha tabia kwa sababu alikuwa ni mraibu wa madawa ya kulevya.

Hata hivyo taarifa anayosema ilikuwa ya kubadilisha ni ile ambayo alimuokoa msichama mmoja kutoka eneo la Kuria kutoka mikononi mwa watu waliokuwa wamemteka nyara na kumuona

Msichana huyo mwenye umri wa miaka kumi na mitatu aliukuwa amechukulia kutoka kao na kuvukishwa mpaka hadi nchini nchini Tanzania punde tu baada ya kuayiwa tohara.

“Kwa kuwa sasa alikuwa ni mtu mzima, alihepeshwa na nilipopata taarifa hizo nilikwenda hadi nchini Tanzania ambako hta nilijipata mikononi mwa polisi wa mpakani walionishika kwa kuingia nchini Tanzania na kufanya taarifa bila ya kibali.

Enzi hizo zilikuwa za marehemu Rais Magufuli na uhuru wa uandishi wa habari ulikuwa umeminywa sana na polisi walinizuia hadi pale nilipowasiliana na upande wa serikali ya Kenya na nikaachiliwa.

Msichana huyo aliungana na wazazi wake na kwa sasa yuko kidato cha tatu katika shule moja ya sekondari katika eneo la Kuria.

Hata hivyo Odee anasema kufuatilia taarifa za kijinsia si kazi rahisi kutokana na vikwazo tofauti tofauti ambayo hukabili hatua hiyo.

“Kwa mfano kunaweza kuwa na ukosefu wa vifaa au fedha za kufuatilia taarifa hiyo mahali iliyopo,” anasema huku akiongezea kuwa mara nyingine upinzani unaweza kutoka kwa wahariri ambao hutilia maanani taarifa za kisiasa kuliko zile za kijinsia

Pia huwa kuna uoga kuwa wale ambao unaowaandikia taarifa wanaweza kukudhuru hasa wakijua kuwa unataka kufichua maovu ambayo wanayafanya.

Mwandishi huyu mwenye umri wa miaka 34 ambaye pia hufanya taarifa za upekuzi anasema kuwa yeye ni mwanafunzi wa uhalisia na ana mengi ya kujifunza kutokana na mikondo ya maisha.

Marafiki zake wanaitakidi kuwa Odee ni mtu ambaye hawezi kuacha fursa ya kutoa taarifa za kuwakomboa kina mama waliodhulumiwa imuondokee

“Odee hawezi lala akijua kuwa kuna haki ya mwanamke mahali fulani ambayo inakiukwa na atahakikisha kwa vyovyote vile kuwa haki inatendeka,” rafiki yake wa karibu Richard Oderi Onchienku anasema.

Nilipomuuliza kumhusu kakake pacha Odee anasema kuwa Dixon ni kiungo muhimu katika maisha yake na yeye humsaidia katika kufanikissha taarifa zake.

Dickson ni mshirika wangu

“Dickson ni mshirika wangu, ni rafiki na mshauri wangu wa maswala ya kiuandishi pia,” Odee anasema kumhusu kaka yake ambaye wanafanana kama shilingi kwa nyingine.

Anakumbuka jinsi walivyokuwa wakiwachanganya wasichana zamani kutokana na sura zao za kufanana huku wengi wao wakiachwa wasijue nani ni nani.

“Mara nyingi ulijipata unasumbuliwa na msichana ambaye anafikir wewe ni yule mwingine,” Anasema huku akicheka masaibu ya enzi hizo.


“Hata hivyo hayo tumeyaacha na sasa tunashughulika na kujenga maisha ya ndoa. Ndugu yangu ameoa kwa muda wa miaka minane sasa na mimi niko katika uhusiano ambapo hivi karibuni nitaoa.”

Nilipomuuliza atataka kukumbukuwa kwa kufanya nini, Odee anasema anataka atambuliwe kama mtu ambaye alisukumia kuimarisha kwa haki za wanawake.

Jamii haiwezi kuwa na maendeleo yoyote yale ikiwa tamaduni potovu na dhuluma dhidi ya wanawake zinakubaliwa kuendelea kutawala,” Odee anaelezea huku akisema ana matumaini kuwa siku moja hili litatimia. Kwa sasa Odee anamiliki jarinda la mtandaoni la Straight news ambako anafuatilia kwa karibu maswala ya kumwezesha mwanamke.
admin

4 thoughts on “Kutana na mwana aliyekataliwa aliyegeuka mtetezi wa haki za kijinsia

Leave a Reply

Your email address will not be published.