Kiswahili kitukuzwe… Sherehe kutambua Kiswahili kama lugha muhimu zaidi ulimwenguni kufanyika Julai 7

Kiswahili kitukuzwe… Sherehe kutambua Kiswahili kama lugha muhimu zaidi ulimwenguni kufanyika Julai 7

Sherehe za kwanza kuadhimisha kutambuliwa kwa lugha ya Kiswahili kama mojawapo wa lugha muhimu zaidi ulimwenguni zitafanyika tarehe saba Julai mwaka huu.

Hii ni baada ya lugha ya Kiswahili kutambuliwa rasmi kama mojawapo wa lugha kumi zinazozungumwa kwa wingi sana ulimwenguni.

Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamadauni (UNESCO) lugha ya Kiswahili inazungumzwa na zaidi ya watu milioni mia mbili kote ulimwenguni.

Soko la Marikiti lililoko Mji wa Kale Mombasa. PIcha: Rolf Dobberstein kutoka Pixabay

Kiswahili ni lugha ya kwanza barani Afrika kutambuliwa na Umoja wa Mataifa na lugha muhimu katika kuendeleza utamaduni, kujitambua, dhamani, na maono ya waswahili.

Yumkini Kiswahili pia kinachangia kuingiliana kwa jamii tofauti, kujielezea na hata kusaidiana na kujengana.

Shirika la makavazi nchini (National Museums of Kenya) kwa ushirikiano na Taasisi ya mafunzo ya turathi (Kenya Heritage Training Institute), wakazi wa mji wa kale, Mombasa,  Shirika la kukuza Kiswahili na Kituo cha Swahili Pot wameandaa sherehe kisiwani Mombasa kusherehekea siku hiyo.

Kwa mujibu wa Mshirikishi wa Shirika la Makavazi Pwani na Taasisi ya Mafunzo ya Turathi na lugha, Khalid Omar Mohamed, sherehe hizo zinanuia kusherehekea na kutambua utamaduni wa waswahili na Kiswahili kwa ujumla.

Baadhi ya vyakula vya Waswahili vitakuwa vinaonyeshwa kwenye sherehe za maadhimisho. Rolf Dobberstein kutoka Pixabay

Vyakula, nyimbo, mashairi na mambo mengine yanayoambatana na utamaduni wa waswahili ni baadhi ya mambo ambayo yatakuwa yanaonyeshwa.

Kiswahili kimetambuliwa kutokana na ukweli kuwa ni mojawapo wa lugha mihimu katika Jumuia ya nchi za Umoja wa Bara Afrika, Muungano wa maendeleo ya Nchi za kanda ya Kusini Mwa Afrika, Jumuia ya nchi za Afrika Mashariki.

Kiswahili kinatambuliwa kama lugha muhimu katika kuendeleza malengo ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo endelevu (Sustainable Development Goals 2030) na kuunganisha nchi za kanda ya afrika mashariki katika kutekeleza makubalinao ya biashara huru katika bara la Afrika (African Continental Free Trade Agreement (ACFTA)

admin

Leave a Reply

Your email address will not be published.