Kipute kitambe, Kivumbi kipande, AFCON 2021 yang’oa nanga.

Kipute kitambe, Kivumbi kipande, AFCON 2021  yang’oa nanga.

Na Edwin Muthomi

Fainali za kombe la mataifa barani Afrika (AFCON) zitang’oa nanga Jumapili usiku baada ya miaka miwili. Michuano hii imeandaliwa nchini Cameroon.

Mtanange wa kwanza, Kundi A, utasakatwa ugani Stade Omnisport Paul Biya, Olembe ambapo wenyeji Cameroon ukipenda ‘Indomitable Lions’ watakuwa wakidhihirisha ukali wao dhidi ya Burkina Faso saa moja jioni (Afrika Mashariki).

Timu hizi mbili zimepatana Mara nne, wakitoka sare tatu, Cameroon kushinda mechi moja Burkina Faso akiambulia patupu kila kukicha.

This image has an empty alt attribute; its file name is 374a1-16415781520503-1920-1024x576.jpg
Wachezaji wa Cameroon. Cameroon Itapambana na Burkina Faso katika mechi ya kwanza. Picha: Kwa hisani ya SportsKeeda

Cameroon wanatajwa kuwa weledi wa kuibukia kileleni mwa Kundi A wakijivunia wachezaji wepesi kama Vincent Aboubakar na Karl Toko-Ekambi.

Burkina Faso Chini ya Kocha Kamou Molu wako katika fomu maridhawa baada ya kutoshindwa katikati mechi saba za hapo awali katika mashindano yote zikiwemo mechi za kufuzu kwa kombe la dunia.

Vijana wake Antonio Oliviera Cameroon watajizatiti vilivyo kuwapa fahari Mashabiki wa nyumbani wakiwa waandalizi wa fainali hizi toleo la thelathini na tatu.

Mshambulizi Bertrand Traore anayepiga soka ya kulipwa na Aston Villa atakuwa kifaa cha kuegemewa upande wa ‘The Stallions’ pamoja na beki Edmond Tapsoba anayetambulika kuwa kisiki na wapinzani.

Kwinginkeko, Vijana kutokea pembe ya Afrika Ethiopia watakuwa wakinadi umahiri wao barani Afrika watakapocheza na Cape Verde ugani Olembe kuanzia saa nne usiku ndani ya kundi A.

Ethiopia Chini ya ukufunzi wake Wubetu Abate watakuwa wakipania kuimarisha matumaini yao ya kufuzu kwa awamu ya maondoano ikibainika dhahiri shahiri ni timu mbili tu zitaweza kuvuka.

Timu zote mbili hazijaweza kukutana hapo awali, licha ya hayo Cape Verde anajivunia kutoshindwa katika mechi nne za awali.

Edwin Muthomi ni mwandishi wa Habari anayeibuka na anayependa kuandika taarifa za michezo, ulibwende na biasharaAnapatikana kupitia barua pepe gurusomi18@gmail.com

admin

Leave a Reply

Your email address will not be published.