Kaulong: Jamii iliyowanyonga wajane ili waandamane na waume zao ahera

Kaulong: Jamii iliyowanyonga wajane ili waandamane na waume zao ahera

Katika dunia hii kuna jamii zenye tamaduni za ajabu, zisizoelezeka, za kushangaza na wakati mwingine zinazokuna vichwa.
Kutana na jamii ya Kaulong iliyoko nchini Papua New Guinea. Jamii hii iliwaua wajane kwa kuwanyonga ili waandamane na waume zao katika maisha ya baadaye ahera.
Kwa mujibu wa wanaathropolojia kitendo hicho kilitekelezwa na shemeji wa kiume wa mjane na kama hangekuwepo basi mtoto wa kiume wa familia hiyo alichukua jukumu kumnyonga mamake.
Kukosa kutekeleza jukumu hilo ilimaanisha ukosefu wa heshima na ilizua taharuki kubwa.
Kulingana na Jared Diamond kwenye kitabu chake The World Until Yesterday mama alikuwa na haki ya kumuuliza mwanawe kumnyonga na akikosa kufanya hivyo basi angeambia jamii kuwa mwana huyo alitaka kulala naye.
Madai hayo yalisababisha aibu kubwa na kumfanya mwana kukosa jingine kumuua mama mzazi.
Diamond anasema utamanduni huo ulisababisha taharuki na madhara makubwa kwa jamii hiyo huku wavulana wakishindwa kuwaua mama zao.
Aidha jamii hiyo ilitekeleza utamaduni huo ambao iliukomesha miaka ya 1950 kwa kuamini kuwa roho za waume waliokufa zilihitaji kuandamana na wake zao ili kuishi maisha ya baadaye yenye furaha na starehe.
Kwa mujibu jariba la Brittanica Papua New Guinea, ni nchi ya visiwa vilivyoko kusini magharibi mwa ziwa la Pacific.
Jarida linasema wakaazi wa jamii tofauti ambazo zinajumuishwa na kuitwa Melanesians walianza kuishi kwenye visiwa hivyo yapata miaka 40,000 iliyopita.
Nchi hiyo ilipata uhuru wake mwaka wa 75 kutoka kwa Australia japo bado iko chini ya utawala wa Malkia wa Uingereza.
Moja wapo wa changamoto zinayoikumba nchi hii ni jinsi ya kuunganisha makabila mengi yenye tamaduni tofauti ili yaweze kuwa taifa moja

admin

Leave a Reply

Your email address will not be published.