Hatimaye Waiguru akataa “kukodishwa” abebwa na wilbaro ya Ruto

Hatimaye Waiguru akataa “kukodishwa” abebwa na wilbaro ya Ruto

Gavana wa Kirinyaga Anne Waiguru amehamia chama cha UDA kinachoongozwa na Naibu wa Rais William Ruto

Waiguru ambaye amekuwa akitoa ishara tofauti tofauti kuhusiana na kuhama chama cha Jubilee hatimaye amepiga moyo konde na kuogelea kwenye lindi la siasa kwa kuamua kufuata mapenzi ya moyo wake.

Waiguru amekuwa akihudhuria mikutano ya kinara wa ODM Raila Odinga na anakumbukuwa kwa msemo wake “kuwa huwezi mnunua mkikuyu ila unaweza kumkodisha kwa muda” matamshi yaliyonuiwa kuonyesha kuwa ufuasi wa watu wa mlima Kenya kwa Ruto ulikua wa muda tu.

Waiguru pia aliwahi sema kuwa kila wakati alipotoa ishara ya kutaka kuhama Jubilee alipata vitisho vya kushtakiwa kuhusiana na sakata za ufisadi alizohusishwa nazo.

This image has an empty alt attribute; its file name is waiguru-aa.png

Naibu wa Rais William Ruto amemkaribisha Waiguru katika chama hicho ambacho kinaonekana  kuwa na wafuasi wengi katika eneo la mlima Kenya hasa kutokana na kile wadadisi wa siasa wanasema ni siasa zake za kuinua mashinani.

Hatua ya Waiguru kuhama Jubilee inatokea siku chache tu baada ya kuandaa sherehe za mashujaa zilizohudhuriwa na Rais Uhuru Kenyatta ambako wananchi walionyesha dhamana yao kwa Ruto.

This image has an empty alt attribute; its file name is 247094070_3009761985903462_697788270954027534_n-1024x682.jpg

Huenda hatua ya Waiguru itaongeza masaibu katika mlengo wa aliyekua waziri mkuu Raila Odinga ambaye amekuwa akitafuta kuungwa mkono na upande wa mlima Kenya hatua ambayo imepigwa jeki na Rais Uhuru Kenyatta.

Hatua hiyo pia inamueka mwakilishi wa kike katika kaunti ya Kirinyaga Purity Wangui Ngirici katika hali ya ati ati hasa ikizingatiwa amekuwa mfuasi mwaminifu na mwasisi wa chama cha UDA.

Mmoja wa wakosoaji wa Waiguru, Dennis Itumbi ametangaza ujio wa Waiguru katika chama cha UDA.

admin

One thought on “Hatimaye Waiguru akataa “kukodishwa” abebwa na wilbaro ya Ruto

  1. Kufikia Februari mwakani, hapo ndipo wakenya watajua msimamo wa wanasiasa. Kwa Sasa wacha waendelee kubebwa na wilibaro wengine wakiendeshwa na azimio la umoja dereva akiwa Tinga

Leave a Reply

Your email address will not be published.