Haiti, taifa ndogo ambalo haliishi misukosuko

Haiti, taifa ndogo ambalo haliishi misukosuko

Haiti ni nchi inayopatikana katika katika eneo la Carribean. Nchi hiyo yenye ukubwa wa kilomita 27,750 mraba ina takriban wananchi milioni 11.4  kwa mujibu wa Benki ya Dunia, (2020)  .

Wengi  wa wananchi wa Haiti ni wa asili ya Kiafrika wakiwa ni vizazi vya waliokuwa watumwa waliofanya kazi katika mashamba ya wazungu.

Haiti ambayo zamani ilikuwa koloni ya Ufaransa ni nchi ambayo inakabiliwa  na misukosuko ya uongozi na utawala mara kwa mara.

Msukosuko wa hivi karibuni ni mauaji ya aliyekuwa rais wa nchi hiyo marehemu Jovenal Moise aliyeuawa na wanamgambo kwa ushirikiano na baadhi ya viongozi kwenye serikali yake.

Kwa sasa nchi hiyo inakabiliwa na mgogoro baada ya wamishionari kumi na saba baadhi yao wakiwa raia wa Marekani kutekwa nyara na magenge ya kihalifu ambayo yamechukua fursa ya kusambaratika uongozi kutekeleza uhalifu.

Mwandamanaji aonyesha ghadhabu zake. Picha: Kwa hisani

Wateka nyara hao wametishia kuwaua mateka wao iwapo hawatalipwa dola milioni kumi na saba ili kuachilia wamishonari hao.

Kwa mujibu wa Benki ya Dunia maendeleo nchini Haiti yanakwamizwa na migogoro ya kisiasa, utawala mbovu na migawanyiko.

Katika mwaka wa 2020 Haiti iliorododheshwa nambari 170 kati ya nchi 189 ulimwenguni kote kuhusiana na maendeleo ya watu. Taifa hilo limebakia nchi  maskini zaidi katika eneo la Latin America na Carribean na ulimwengu mzima kwa jumla

Mambo kumi muhimu kuhusu Haiti

  1. Mji wake mkuu unaitwa Port-au-Prince
  2. Nchi hii ilikuwa koloni ya Ufaransa na ilipata uhuru wake mwaka 1804.
  3. Asilimia 60 ya wakazi wa Haiti ni maskini
  4. Takriban 60% ya wananchi wa Haiti ni watu wachanga wakiwa na umri kati ya miaka 15 hadi 64
  5. Taifa hili linakabiliwa na majanga ya kimaumbile huku asilimia 96% ya wakazi wake wakiwa katika hatari ya kuathirika kila wakati.
  6. Mnamo mwaka wa 2016 kimbunga Mathew kiliharibu takriban asilimia 32 ya uchumi wa nchi hiyo
  7. Tetemeko la ardhi la mwaka wa 2010 liliua watu wapatao 250,000.
  8. Haiti ni nchi iliyogawanyika kisiasa na kijamii na ingawa wengi wanatamani demokrasia hili bado ni ndoto kwao.
  9. Rais wa sasa wa Haiti ni Claude Joseph aliyeteuliwa kama waziri mkuu na kisha kuchukua wadhifa wa kaimu rais  Julai 7 2021 hadi 20 Julai 2021.
  10. Dini ya kikatoliki na mila za asili ya Kiafrika za Vodudou ndio zinazotawala imani katika taifa la Haiti.

admin

Leave a Reply

Your email address will not be published.