Gharama ya urembo: Wanawake wavaa visigino virefu kuimarisha urembo

Gharama ya urembo: Wanawake wavaa  visigino virefu kuimarisha urembo

Jalida la Forbes linakadiria kuwa wanawake hutumia zaidi ya dola bilioni 20 kila mwaka kununua viatu peke yake. 

Kwa mujibu wa takwimu mwanamke mmoja anaweza miliki kati ya jozi 19 hadi 34 huku mwanaume akiwa na kati ya jozi saba hadi 12 za viatu.

Ukweli ni kuwa vingi ya viatu vya wanawake ni vile vyenye visigino virefu.

Visigino virefu huimarisha umbo

Kulingana na watafiti wa mitindo ya viatu, na wanaanthropolojia wanawake wanapenda viatu vyenye visigino virefu kutokana na sababu kadha wa kadha

Kwa mfano kulingana na mwandishi John Updike, viatu vyenye visigino virefu huimarisha urembo wa mwanamke kwa vile huufanya mgongo wake kuonekana uliojikunja vyema.

Matembezi ya mwendo wa madaha pia ni kitu ambacho hufanya viatu vyenye visigino virefu kupendwa na wanawake.

Visigino virefu huimarisha umbo. Picha kwa hisani

Aidha uchunguzi wa wasomi nchini Ufaransa uling’amua kuwa wanawake walivutia zaidi wanaume kadri urefu wa kisigino cha kiatu ulivyoongezeka.

Kulingana na utafiti huo asilimia 82 ya wanaume walikuwa tayari kushiriki katika uchunguzi ulioendeshwa na wanawake wenye kuvaa viatua vyenye visigino virefu  ikilinganisha na asilimia 60 na 42 ya wale waliovaa visigino wastani na waliovaa viatu visivyokuwa na visigino.

Kwa mujibu wa historia, viatu vyenye visigino virefu vilivaliwa kama ishara ya kuonyesha nafasi na tabaka la mhusika katika jamii. Ingawa viatu hivi vilivaliwa na wanaume kwa wake kwa pamoja, sura ya kiatu ilibadilishwa ili kutofautisha kati ya wake na waume.

Aidha watu waliotoka jamii za kiutawala walivaa visigino virefu kujitofautisha na watu wengine wasiokuwa na tabaka na waliokuwa wafupi walipata fursa ya kutoshana na wale warefu na kuweza kuwaangalia uso kwa uso.

Wawawake waliokaa kwenye nyumba za kifalme kwa minaili ya kutumika kuwastarehesha wafalme nao walivaa visigino virefu kuongezea urembo wao na kuwanya kuvutia na hata kuwasiliana na watu wengine kwa njia tofauti hali iliyowapa nguvu na kujiamini.

Athari ya visigino virefu

Ingawa visigino virefu vinaweza kuuumiza miguu kwa kufinya vidole kutokana na undogo wake na kuvaliwa kwa muda mrefu, wanawake wengi bado wanapenda kuvivaa.

Kwa mujibu wa Shirika la Matabibu wa mifupa nchini Marekani American Academy of Orthopaedic Surgeons, tisa kati ya wanawake kumi hukiri kuwa visigino virefu vinaumiza na hata kuleta athari za kiafya.

Mwanamke aliyeumizwa na visigino virefu Picha: Kwa hisani

Lakini hilo si jambo linalowashtua wanawake kwani vinawasaidia kuuza urembo wao kama vile watu wa jamii za kifalme, makahaba na wale ambao wanauza mitindo ya mavazi wanavyofanya.

Yumkini msomi Elizabeth Semmalhack anasema urefu wa kisigino huoongezeka na kupungua kutokana na hali ya kiuchumi. Uchumi unapofanya vyema kisigino hurefuka na uchumi unapoporomoka, urefu wa kisigino hupungua.

Lakini je, kisigino kirefu huchangia nini?

  • Kisigino kwanza huwa kinavutia wanaume
  • Matiti ya mwanamke huonekana makubwa. Kwa kuwa mgongo hujipinda kidogo, matiti hujivuta mbele na kuonekana yanayovutia jambo ambalo hupendwa na wanaume wengi.
  • Makalio ya mwanamke huonekana makubwa kwa sababu yameinuliwa na kisigino na hili nalo huvutia wanaume sana.
  • Mwanamke anapotembea kiuno na makalio huonekana kucheza zaidi kutokana na hatua ndogo ndogo ambazo mwanamke anapiga anapotembea kwa makini asije akajikwaa ama kuanguka
  • Miguu ya manamke huonekana midogo na wanaume wanavutiwa sana na miguu midogo ya wanawake.

Ingawa hivyo visigino hivi vina gharama kubwa kutokana na bei, majeraha kwenye miguu, kuumiza mishipa na hata uchungu mgongoni.

Lakini wanawake wengi wako radhi kusahau haya yote na kuvaa visigino virefu almuradi tu wabaki kuwa warembo.

admin

2 thoughts on “Gharama ya urembo: Wanawake wavaa visigino virefu kuimarisha urembo

  1. Maelezo mazuri sana. Nilishangaa mwanamke mmoja aliponieleza kuwa kuvalia viatu vyenye visigino virefu ama ukipenda RAIZONI kuwaongeza ujasiri (confidence)

Leave a Reply

Your email address will not be published.