Fuata nyuki ule….chakula. Uhaba wa nyuki waanza kuathiri uzalishaji chakula

Fuata nyuki ule….chakula. Uhaba wa nyuki waanza kuathiri uzalishaji chakula
This image has an empty alt attribute; its file name is corn-2655525_960_720.jpg
Zao la mahindi shambani. Wakulima wanatumia mikono kuchafuza mimea kutokana na uhaba wa wadudu muhimu

Na Victor Moturi

Utumizi wa madawa ya kuua wadudu waharibifu na magugu shambani umepelekea upungufu wa wadudu muhimu ambao huchangia uchavushaji yaani pollination ambayo ni muhimu katika uzalishaji  wa chakula.

Madawa  hayo yana kemikali ambazo huua tu sio magugu na wadudu waharibuiu pekee mbali pia wadudu muhimu kama vile nyuki, vipepeo na wengineo.

Naili kukabiliana na hali hii wakulima wameanza kutumia mikono yao kuchavisha mimea ili kuongeza mazao.

Kulingana na wataalam wa kilimo, uchavushaji yaani pollination ni pale ambapo chembechembe za poleni zinasambazwa kutoka kwa mmea mmoja hadi mwingine kuzalisha mbegu.

Wadudu kama vile nyuki na vipepeo huchangia sana kusambaza poleni shambani. Kwa mujibu wa  Joseph Mbithi ambaye ni baba wa watoto watatu, alianza kutumia mbinu hii baada ya kushuhudia mazao duni kwenye shamba lake.

“Unyunyuziaji wa kemikali za kukabaliliana na magonjwa ya mimea shambani umeathiri njia za kawaida za uchavushaji. Wakulima wengi sasa wanakutumia brashi, mswaki na sifongo yaani sponge kusambaza poleni kutoka kwa mmea mmoja hadi mwingine” Mbithi anasema

Aina za uchafuzi

Daktari Faith Toroitich ambaye ni mtaalam wa kilimo na wadudu katika chuo kikuu cha Egerton anasema kuna aina tatu za uchavuzi, yaani poleni kupaa kutoka kwa ua moja hadi ua lingine kwenye mmea mmoja, na kuna  uchavuzi  baina ya mimea tofauti yaani cross pollination ambapo poleni kutoka mmea mmoja hupaa hadi mmea mwingine. Kunayo mimea hutegemea upepo, wanyama na mimea mingine hutegemea usaidizi wa mikono ya binadamu.

Mimea kama vile maembe, tango yaani cucumber,tikiti maji ,ndimu na limau hutegemea sana nyuki na wadudu wengine kwa uchavushaji ilhali familia ya mimea kama vile Sukuma wiki, mchicha hutegema huchavushaji binasfi yaani self- pollination.

Mimea aina ya mahindi, mtama, ngano, karoti ndizi sana sana hutegemea upepo kwa uchavushaji.

Samuel Nderitu mkulima na mkufunzi wa kilimo katika kaunti ya Kiambu amekuwa akitumia mswaki kusambaza poleni kwenye mimiea yake aina ya Malenge.

Anadokeza kuwa kwa kipindi cha miaka minne shamba lake limekuwa likitoa mazao machache ikilinganisha na miaka ya hapo awali.  Nderitu aligundua amekuwa akitumia kemikali kupita kiasi baada ya maafisa wa kilimo kumtembelea shambani mwake.

Nderitu anasema anachavuza takribani mimea 100 huchavushwa kila siku kwa kutumia mswaki, huku wanafunzi ambao hufurika hapa wakichangia pakubwa kutekeleza shughuli hii nzima.

Hata hivyo kubadilika kwa tabia nchi yaani climate change, pia kumechangia pakubwa kuathirika kwa mimea ambayo hutegemewa sana na wadudu wanaochavusha hivyo wadudu hao kuangamia.

Mtalaam wa wadudu Daktari Toroitich anashauri kuwa kuimarisha mazingira kutasaidia ongezeko la wadudu kama vile nyuki na vipepeo shambani.

Umuhimu wa wadudu

Daktari Sunday Ekesi ambaye ni mtaalam katika kituo cha kimataifa  cha utafiti wa wadudu yaani International Centre of Insect Physiology and Ecology (ICIPE), anasema Asilimia 75 ya mimea inahitaji uchavuzi kupitia wanyama, wadudu na hata upepo.

“Thamani ya uchavuzi ulimwenguni ni kati ya dola  billioni 235 hadi dola billioni 577 kila mwaka. hiyo ni thamani kubwa sana na inaonyesha kuwa bila uchavuzi yaani pollination hakutakuwa na chakula.’’ Ekesi anasema

 “Wakulima katika nchi kama vile Tanzania, Senegali, Burkina Faso, Visiwa vya Komoro na Nigeria tayari wanachavusha mimea kutumia mswaki au brashi shambani huku wengine wakilazimika kufuga wadudu pamoja na kusindika mizinga kando kando ya mashamba ili kuwavutia nyuki,” anasema Ekesi .

Mwaka jana wakulima nchini Kenya wakishirikiana na vikundi vya kuboresha ukulima, waliliomba bunge kupiga marufuku uagizaji wa  madawa  hatari kwa mimea. Madawa hayo ni kama vile Round-up Pamoja na Malathion ambayo yana chembechembe za sumu.

Kulingana na shirika lisilo la kiserikali la Route to Food, hitaji la madawa ya kunyunyuzia mimea shambani liliongezeka kutoka tani 6400 mwaka wa 2015 hadi tani 15,000 mwaka wa 2018.

Victor Moturi ni mwandishi mahiri kutoka mjini Nairobi ambaye ameshinda tuzo kadhaa kutokana na taarifa anazoandika kuhusu afya na kilimo katika eneo la Afrika Mashariki

admin

Leave a Reply

Your email address will not be published.