Familia yalilia haki, yuko wapi Profesa Nandwa?

Familia yalilia haki, yuko wapi Profesa Nandwa?

Familia na washirika wa msomi Profesa Hassan Nandwa al-maarufu Wilson Nandwa imelilia haki ikitaka kujua mahali alipo baba yao

Al-Mikidad Hassan Nandwa mwanawe msomi huyo ameongoza familila kutaka kujua mahali alipo baba yao ambaye wanashuku alitetwa nyara na askari polisi kutoka makazi yake ya Ngong Road mjini Nairobi.

Profesa Nandwa ni wakili na msomi katika chuo kikuu cha Umma na anasemekana kutekwa nyara Alhamisi wiki hii

Familia imesema imemtafuta katika kila kituo cha polisi bila kumpata baba yao ambaye pia ni mtetezi wa haki za kibinadamu.

Mkurugenzi mkuu wa Shirika la kutetea haki za kibinadamu la Haki Africa Hussein Khalid amesema kutekwa nyara kwa Profesa Nandwa ni ukiukaji mkubwa haki za kibinadamu.

Familia inasema kama kuna makosa ambayo msomi huyo alifanya anastahili ashtakiwe rasmi lau sivyo serikali imtoe mahali alipo.

Tayari chama cha wanasheria mjini Nairobi kimemkashifu utekai nyara wa Nandwa na kikataka aachiliwe.

Prof Nandwa ni wakili mshtakiwa Joseph Jowie Irungu katika kesi ya mauaji ya Monica Kimani aliyepatikana akiwa amekatwa shingo katika nyumba yake iliyoko Lamuria Garden eneo la Kilimani mwaka wa 2018

admin

Leave a Reply

Your email address will not be published.