Fahamu jinsi Ua-janja linavyowakomesha ndovu Laikipia

Fahamu jinsi Ua-janja linavyowakomesha ndovu Laikipia

NA Victor Moturi

Wakazi wa Mathira katika kaunti ya Laikipia wana kila sababu ya kutabasamu baada ya kuwekewa ua-janja ambalo litawazuia wanyama kuharibu mimea yao na kupunguza migogoro kati ya binadamu na wanyama.

Mgogoro huu umepelekea kuuawa kwa binadamu, wanyama na uharibifu wa chakula hasa wanyama wanapoingia shambani.

Ua-janja lenye nyaya zinazowadungadunga ndovu huwazuilia kuingia shambani


Kulingana na wakulima katika eneo hilo wanyama hao huvamia mashamba yao kwa wingi huku wakiharibu chakula na hata kuhatarisha maisha ya binadamu na mifugo

Francis Kamau, mmoja wa wakulima katika eneo hilo anasema ndovu wanasababisha hasara kubwa wanapovamia mashamba.

Wakulima eneo hilo sasa wana sababu ya kutabasamu baada ya shirika moja lisilo la kiserikali kuwawekea ua-janja ambalo linazuia wanyama kufika shambani.

Ndovu wakiwa mbugani. Ua-janja huwatambua wanaosumbua na kuwezesha kuwafuata na kuwaweka vidhibiti

Kwa mujibu Alice Mukami ambaye ni mkulima eneo hilo sasa wanaweza kutekeleza kilimo bila wasiwasi kwani kuna vile idara ya wanyama hufahamu kabla ya wanyama kufika shambani.

“Sasa tumepanua mashamba yetu, mavuno yetu tunaona yanaendelea vizuri,’ Anasema Mukami.
Ua- janja hilo lenye urefu kilomita 125 liliwekwa kwa ushirikiano la shirika lisilo la kiserikali la Spaces for Giants.

Ua-janja hili linatumia aina ya nyaya fupi zenye umeme ambazo humdunga-dunga ndovu anapojaribu kuingia shambani.

Kisha ua-janja hilo hutuma jumbe za kuingiliwa na ndovu kupitia kwa njia ya setilaiti na hivyo kuwezesha maafisa wa wanyama kuingilia kati na kujaribu kuwaondoa ndovu.

Mimea inanawiri shambani baada ya sehemu hiyo ya Mathira kuwekwa ua-janja


Ua-janja hilo pia linatumia kamera janja ambazo ambazo hutuma ujumbe na hata kuwatambua ndovu wanaosumbua kwa nia ya kuwaweka vidhibiti vya kufahamisha mahali walipo.

Eneo la Laikipia linakadiriwa kuwa na ndovu wapatao 4700 ambao wanaishi katika mbuga na mashamba ya uhifadhi wa wanyama pori.

Victor Moturi ni mwandishi mahiri kutoka mjini Nairobi ambaye ameshinda tuzo kadhaa kutokana na taarifa anazoandika kuhusu afya na kilimo katika eneo la Afrika Mashariki

admin

Leave a Reply

Your email address will not be published.