Ethiopia yaweka amri ya kutotoka nje kukabili TPLF

Ethiopia yaweka amri ya kutotoka nje kukabili TPLF

Serikali ya Ethiopia imetangaza hali ya hatari huku ikiwahimiza wananchi mjini Addis Ababa kujitayarisha kuutetea mji wao kutokana na tishio la wanamgambo wa Tigray ambao wanakaribia mji huo mkuu.
Kwenye hali hiyo ya hatari maagizo ya kutotoka nje, kufungwa kwa barabara na kupekuliwa kwa watu ambao wanahofiwa kushirikiana na makundi ya kihalifu yatatakelezwa.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Fana, serikali itakuwa na uwezo wa kumlazimisha mtu yeyote aliye na umri wa kupigana na mwenye silaha kujiunga na jeshi. Pia serikali itafunga vituo vyote vya habari ambavyo huenda vikashirikiana na wanamgambo wa TPLF
Mzozo huo unatokana na taarifa kuwa wana mgambo hao wa TPLF ambao wamekuwa wakikabiliana na serikali inayoongozwa na Dr. Abiy Ahmed wanakaribia mji huo mkuu.

Mnara wa wahanga katika mii mkuu Addis Ababa. Mnara umewekwa kusherehekea maelfu ya watu waliofariki wakipigania uhuru wa nchi yao

Serikali ya Ahmed ilishambulia eneo la Tigray Novemba mwaka uliopita na kupelekea kuwepo kwa janga la kibinadamu kwani maelfu ya watu walifariki huku wengine wapatao milioni 1.5 wakihamishwa makwao.
Serikali hiyo pia ilikataza mashirika ya misaada kupeleka chakula katika eneo hilo licha ya shinikizo la kuwa watu walikuwa wanataabika.
Mwezi Julai Ethiopia iliwafukuza maafisa watano wa Shirika la Umoja wa Mataifa baada ya kuitaka serikali kufungua njia na barabara ili kuwezesha kupelekwa msaada kwa watu wanaoadhirika na baa la njaa katika eneo la Tigray
Mzozo huo pia umepelekea Marekani kuiondoa Ethiopia katika mwafaka wa biashara wa AGOA kama nia ya kuishinikiza serikali ya Ahmed kuweka mikakati ya amani.
Mwafaka huo huiletea Ethiopia kima cha dola milioni 100 kila mwaka na kusababisha kuajiriwa kwa watu wapatao elfu 100.
Kulingana na Banki ya Dunia Ethiopia yenye wananchi milioni 112 ndio nchi ya pili yenye idadi kubwa ya watu barani Afrika baada ya Nigeria.
Hata hivyo Ethipoia nia mojawapo wa mataifa maskini zaidi huku ikikabaliwa na changamoto za kukuza uchumi wake, kupunguza umaskini na kuunda nafasi za ajira kwa idadi yake kubwa ya vijana.
Kulingana na Shirika la Human Rights Watch hali ya usalama imeendelea kuzorota kadri waziri  mkuu wa nchi hiyo Abiy Ahmed alivyojaribu kuweka amani.
Hali hii ilipelekea kutokea mandamano na mzozo ya kisiasa huku vikosi vya serikali, makundi ya kiharamu yaliyofuata mikondo ya kikabila na kijamii yakilaumiwa kwa kuwashambulia wananchi
Mzozo wa Ethiopia unasemakana kuzungukia katika maswala tata kuhusu ardhi, siasa na ukabila.

admin

Leave a Reply

Your email address will not be published.