Ero, wewe leta tu mbuzi, tapata afya bora

Ero, wewe leta tu mbuzi, tapata afya bora

Na Victor Moturi

Kaunti ya Kajiado imezindua mbinu mpya inayonuiwa kuwashinikiza wakazi wa kaunti hiyo hasa wa jamii ya kimasai kujiunga na bima ya afya ya taifa NHIF.

Hatua hii inanuiwa kuhakikisha kuwa wengi wa wananchi wako chini ya mwavuli wa NHIF ili kuwaondolea mahangaiko wakati wanapougua.

Mpango huo unaojulikana kama mbuzi mmoa afya bora unawasaidia wakazi hao kujisaili kwa bima ya afya kwa kutumia mbuzi.

Simon Saidemo baba a watoto wanne anasema  tangu ajiunge na mbuzi moja afya bora ameona faida kwani ashawahi kutibiwa kwa kutumia kadi ya bima hiyo.

Saidemo anawahimiza wananchi kujiunga na mpango huo ili kuepuka gharama kubwa za hospitali

Mmoja wa wafugaji na mbuzi wake

“Wito wangu ni kuwa wananchi wajiunge na bima ile wafanye mambo yao ikuwe rahisi na kuwezesha kuepuka na mambo ya gharama ya bill ya hospitali, ,” anasema.

Gharama ya bima ya taifa ni shilingi elfu sita na mbuzi mmoa anatosha kulipia gharama hiyo kwa muda wa mwaka mmoja.  Hata hivyo wananchi wanahitajika kulipa fedha katika mwaka unaofuata

Mpango wa mbuzi mmoja umewawezesha wananchi wengi katika kaunti hiyo ambao walikuwa hawana pesa taslimu kujisajili katika bima ya afya ya taifa.

Kwa mujibu wa maafisa wa serikali ya kaunti ya Kajiado mpango huo umewafaidi zaidi watu 5000 tangu ulipozinduliwa mwaka wa 2018.

Kulingana na Samson Saigilu, mkurugenzi wa matibabu katika kaunti hiyo mpango huo unasaidia jamii za eneo hilo ambazo zinategemea sana madawa ya kiasili ya mitishamba.

Victor Moturi ni mwandishi mahiri kutoka mjini Nairobi ambaye ameshinda tuzo kadhaa kutokana na taarifa anazoandika kuhusu afya na kilimo katika eneo la Afrika Mashariki

admin

Leave a Reply

Your email address will not be published.