Eric Omondi amruka Maribe: “Sina uhakika mtoto ni wangu”

Eric Omondi amruka Maribe: “Sina uhakika mtoto ni wangu”

Mzozo kati ya wapenzi wawili wa zamani unaendelea kutokota huku wakilaumiana kwa kukosa kuwajibika vilivyo.
Kwa upande wake Maribe anadai Omondi hajawahi shughulikia mwanae wa kiume mwenye umri wa miaka saba huku naye Omondi akidai hana uhakika kama yeye ndiye baba wa mtoto.
Mzozo huo ulianza pale Omondi alipotangaza kuwa amemtia msichana mmoja mimba na kuahidi kumshughulikia.
Haikujulikana mara moja kama Omondi alikuwa anaendeleza matani na kukipa kipindi chake cha “wife material” cheche na haiba.

This image has an empty alt attribute; its file name is Eric-a.png
Usemi wa Omondi katika mtandao wake wa Instagram

Hata hivyo Maribe alionekana kumzoma Omondi huku akisema hana uhakika atawajibika vilivyo.
Omondi sasa ameurusha mpira kwa Maribe akisema hana uhakika kama yeye ndiye baba wa mtoto huyo wa Maribe na licha ya kutaka kujua ukweli Maribe alimkatalia.
Omondi pia anamlaumu Maribe kwa kuwa na wapenzi wengine walipokuwa wanajuana na hilo linatilia shaka kama yeye ndiye baba wa mtoto

Usemi wa Omondi katika mtandao wake wa Instagram


“Tulifanya mapenzi siku moja tu baada ya sherehe kwenye kampuni ya Radio Africa na kwa kutumia kinga na vile ambavyo Maribe alisema nilimtia mimba bado ni kuzungumkuti kwangu.
Baada ya miezi miwili aliniambia ana mimba na mimi ni babake mtoto. Nilipomuambia tulifanya mapenzi kwa kutumia kinga alisema mama siku zote hujua nani baba ya mtoto.
“Kama unataka niwaijibike basi tukaanye kilicho cha sawa tukapime DNA,” akasema Omondi.
Mgogoro huu umewavutia baadhi ya watu maarufu akiwemo Akothee anayemwambia Maribe amshughulikie mtoto wake bila kumjali Omondi kwani kumfuatilia kutamvunjia raha na amani yake ya kuwa mama. Akothee anasema kama mama wa watoto watano alipata amani tu baada ya kuacha kukimbizana na baba za watoto wake

Alichoandika Akothee kwenye mtandao wake wa Instagramadmin

Leave a Reply

Your email address will not be published.