Eliud Kipchoge ashinda tuzo jingine ..

Eliud Kipchoge ashinda tuzo jingine ..

Mkimbiaji nguli Eliiud Kipchoge ametangazwa kuwa mwanamichezo bora zaidi katika michezo ya Olimpiki iliyokamilika mjini Tokyo Japan yapata miezi miwili iliyopita

Tuzo hilo la Kipchoge limetolewa na ushirika wa kamati za olimpiki kote ulimwenguni katika kikao kilichofanyika nchini Ugiriki Jumapili tarehe 24 Oktoba

Kipchoge ambaye alikuwa kinara wa Team Kenya kwenye michezo hiyo ni mmoja wa wanariadha waliowahi kushinda medali katika michezo wanayoshiriki kwa kwa mara mbili mfululizo.

Akipokea tuzo hilo Kipchoge alisema kuwa ni heshima kubwa sana kushinda tuzo hilo.

“Ingawa kulikuwa na wanariadha wengi wazuri nimefurahi sana kupokea tuzo hili. Asanteni sana kwa mchango wenu” aliandika kwenye mtandao wa wake wa Facebook.

Kipchoge kwenye mtandao wake wa Facebook

Rais Uhuru Kenyatta amempongeza Kipchoge na kusema tuzo hilo ni kutambuliwa kwa taifa la Kenya kama lenye wanariadha shupavu.

“Ningetaka wanariadha wengine kumuiga Kipchoge ambaye hujitolea, ni mpole mwenye bidii na uzalendo katika ujenzi wa taifa,” Uhuru amesema.

Hongera ya Rais Kenyatta kwake Kipchoge

admin

One thought on “Eliud Kipchoge ashinda tuzo jingine ..

Leave a Reply

Your email address will not be published.