Dubai kimeumana, hakuna usafiri, visa zimeisha, wahamiaji wageukia ukahaba

Dubai kimeumana, hakuna usafiri, visa zimeisha, wahamiaji wageukia ukahaba

Mamia ya wahamiaji katika Jumuia ya Milki za falme za kiarabu UAE wamelazimika kukaa kwenye bustani moja mjini Dubai baada ya muda wa vyeti vyao vya usafiri kuisha.

Wahamiaji  hao hawajaweza kuvilipia na wengi wamebanwa na faini kubwa ambazo zimekuwa kikwazo kikuu kwa wao kupata kazi.

Kwa mujibu wa mkazi mmoja nchini humo ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa sababu za kiusalama, wengi wa wahamiaji hao sasa hawawezi kupata kazi bila visa inayowaruhusu kuwa nchini humo.

Wengi wa wahamiaji hawa ni kutoka nchi za Africa kama Kenya, Ghana, Uganda, Congo, Sudan, Egypt, Ghana, na pia bara Asia kama vile Pakistan, India na kwingineko.

Matamanio ya wengi sio kurudi nchini kwao mbali wangetaka kuruhusiwa kuendelea kufanya kazi nchini humo, akasema mfahamishai wetu.

Kampuni ya ndege ya UAE. Visa za wahamiaji wengi zimeisha muda wa kukaa na hawawezi kusafiri kurudi makwao baada ya nchi hiyo kusitisha usafiri wa ndege.

Baadhi yao wameyaomba mataifa yao kuwapatatia usaidizi warudi makwao kwani kwa sasa wanakumbana na changamoto za ukosefu wa chakula, bima ya matibabu, na mahali maalumu pa kulala.

Nchi hizo za UAE pia ziko kwenye msimu wa baridi na hili linaongeza masaibu ya wahamiaji wasio na mahali maalum pa kukaa.

Moja wapo wa vitu muhimu katika nchi hiyo ni nyumba, chakula na pesa ya nauli kutafuta kazi

Kwa mujibu wa mfahamishai wetu wengi wa waadhiriwa hawa ambao asilimia themanini hususan ni wasichana wamelazimika kujitoza kwenye ukahaba kutosheleza mahitaji yao ya msingi.

Himaya ya milki ya kiarabu ilisimamisha usafiri wa ndege kwa mataifa kadhaa barani Afrika katika siku ya mkesha wa Krismasi mwaka uliopita kutokana na hofu ya kuenea kwa maradhi ya corona.

Nchi hiyo iliongeza muda huo siku chache baadaye na kutia ndoa usafiri wa wahamiaji wengi walionuia kujiunga na familia zao ama kurudi kazini nchini humo.

admin

Leave a Reply

Your email address will not be published.