Bamburi Fisheries, mtaa mdogo unaoifanya Mtwapa ione aibu

Bamburi Fisheries, mtaa mdogo unaoifanya Mtwapa ione aibu

Katika siku za hapo nyuma, safari ya kwenda Pwani ya Kenya haingekamilika kama mtalii hangetembelea mji mdogo wa Mtwapa, ulioko pembezoni mwa kaunti ya Mombasa na Kilifi.

Mtwapa ulijulikana kama mji usiolala, mji wa raha, ufuska na uroda.

Wakati nchi nzima ilipokamilisha shughuli zake za siku na kwenda kulala, Mtwapa ndio ilikua inaupangusa uso, kuchukua kiamsha kinywa chake na kuingia kazini.

Wasichana wa kila aina, wanene ka wadogo, weupe kwa weusi, warefu kwa wembamba walionekana pembezoni mwa barabara wakingojea wateja.

Vilabu vya Mtwapa navyo vilijaa takribai kila siku ya wiki, vilipiga ngoma usiku kucha, huku wazee kwa vijana, wananchi kwa wageni wakipiga sherehe bila kujali kesho.

Watalii wa asili ya kizungu nao wakafahamu raha ya mji huu na wengi wakatoka kwao kuja kujiliwaza kwa kupata joto la jua na la penzi la wasichana wengi waliotoka kila sehemu ya nchi na waliotaka kupendwa na wazungu.

Wakati mwingine vita vilitokea kati ya wasichana hao waking’ang’ana kuhusu wizi wa wapenzi na hasa mababu na vinyanya vya kizungu. Na nguo fupi ambazo wanavaa zilifanya sinema ya bure ya vita kuvutia.

Lakini, tangu serikali ilipopitisha katiba mpya na kuanza mfumo wa ugatuzi, Mtwapa nayo haikuachwa nyuma kwani iligatua ufuska na uroda hadi katika mtaa wa Bamburi Fisheries ulioko kama kilomita tatu kusini mwa Mtwapa na katika kaunti ya Mombasa.

“Hepi hupatikana sana Mtwapa, lakini wanaBamburi walipodai hepi kwa wingi, huduma hii muhimu ililetwa mashinani,” anasema Roy mkazi mmoja wa Bamburi.

Ukiutazama mtaa Fisheries ni mtaa wa kawaida tu, unaokua kwa kasi, lakini hepi zinazoendelea humu, kuanzia majumbani, vilabu, mikahawa na hata kumbi za starehe si chache

 “Hauhitaji tena kwenda Mtwapa kutafuta starehe. Sherehe inayopigwa hapa sasa ni tosha,” anasema Mariamu ambaye zamani alikuwa anaanya kazi Mtwapa

Mtaa huu sasa unawavutia wageni kutoka bara na wale wa mataifa ya nje wakiwemo Wanigeria maarufu kama Wanaija.

“WaNigeria wanajua kufuata sherehe na wamegundua mtaa huu umejaa raha. Hivyo utawaona wameandamana na wasichana wa humu nchini ambao ni wapenzi wao”.

Na wakazi wa Mombasa wana mengi ya kusema kuhusu mtaa huu

Hata hvyo baadhi ya watu wanahofia kuwa kuingiliwa na wageni, kuwepo kwa sehemu nyingi  za starehe na mapenzi ya kiholela ni vitu ambavyo vinaweza changia ongezeko la uhalifu, kuenea kwa maradhi kama vile UKIMWI.

“Kuna uwezekano wa ongezeko la utumizi wa mihadarati hasa kutokana na kuwepo kwa wageni ambao baadhi yao wanajulikana kwa kufanya  biashara ya ulanguzi wa madawa ya kulevya,” anasema Peter mkazi mmoja wa mtaa huu.

Wakazi pia wanasema visa vya mivutano ya kimapenzi ni vingi hasa ikizingatiwa kuwa wasichana wanaoishi Bamburi wana tabia ya kupendana na watu wengi kwa wakati mmoja.

This image has an empty alt attribute; its file name is Capture-2.png

Mmoja anapogudua kuwa anachezwa na yuko kwenye mapenzi ya watu wengi inamkasirisha na kupelekea kuwepo kwa migogoro mingi ya kimapenzi.

Afisa mmoa wa polisi kutoka kituo cha polisi cha Bamburi ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa sababu hana mamlaka ya kuongelea maswala ya polisi amesema wanapokea visa vingi sana vya migogoro ya kimapenzi.

“Tunaandikisha kati ya visa vitano hadi kumi vya mivutano ya kimapenzi kila wiki,” afisa huyo anasema huku akiongeza kuwa baadhi ya visa hivyo ni vya wizi na dhuluma za kijinsia.

admin

Leave a Reply

Your email address will not be published.