Akili mwigo, teknolojia inayosoma na kufasiri tabia yako

Akili mwigo, teknolojia inayosoma na kufasiri tabia yako

Taswira ya kwanza
“Ni nani alikuwa anatumia mashine yangu wakati nilikuwa siko ofisini?” Jamaa mmoja alisikika akifoka punde tu baada ya kurudi kutoka likizo.
“Kwa nini?” Mwenzake akamuuliza.
“Ni kwa sababu ya picha ambazo nazipokea kwa sasa ambazo mimi sina uhusiano nazo.”

Taswira ya pili
“Niliingia mtandaoni kutafuta jinsi ya kuepuka madeni na kilichonishangaza ni kuwa matangazo kuhusiana na App za kukopesha yalianza kumwagika kwenye ukurasa wangu,” Akasema binti mmoja mrembo aliyekuwa anakabiliwa na wakati mgumu kifedha.
“Nilishindwa hata ni kwa njia ipi naweza kuyasimamisha maana yaliongezeka kutoka kila upande.”

Kile ambacho jamaa wa kwanza hakujua ni kuwa hakuna mtu mwingine aliyetumia mashini yake ila ni kile ambacho alikuwa anakifanya kwingine kilikua kinajidhihirisha kwenye mashini yake ya ofisini.

Simu, kompyuta ya nyumbani na ile ya ofisini zilunganishwa kwa pamoja chini ya jina moja ama anauni ya barua pepe na iliwezesha kudukua tabia ya mhusika mtandaoni bila yeye kufahamu kwa kuwa tayari alikuwa ashatoa idhini ya kudukuliwa taarifa zake
Kile ambacho ndugu hawa hawakifahamu ni kuwa teknolojia ya mtandaoni inatumia tabia ya mhusika mtandaoni kujua anachopenda, vitu anavyoepnda kununua, picha na video anazopenda kuangalia na kadhalika.

Baadhi ya watetezi wa haki za wateja wanasema tabia ya udukuzi humuacha mtumizi akiwa uchi hasa kutokana na watu wengine kufahamu tabia yako katika sehemu ambayo inahitajika kuwa ya usiri wako.
Wataalamu wa komputa wanaita teknolojia hii Artificial intelligence ama Akili Mwigo na ina uwezo sio tu wa kujumlisha tabia yako mtandaoni mbali pia kusaidia katika kusuluhisha shida zinazowahusu wateja wa kampuni.

Umuhimu wa Akili Mwigo

Teknoloia hii ina uwezo wa kutoa majibu ya haraka kwani hukusanya taarifa nyingi kwa wakati mmoja, kuzijumulisha na kisha kutoa suluhu za haraka.
Kulingana na Kampuni ya Oracle Kenya teknolojia ya Akili Mwigo inawezesha mashini kuiga akili ya binadamu na kufanya kazi kulingana na taarifa zinazokusanya kuhusu wahusika.
Tabia hii inahusu kukadiria kwa hali ya juu na kufasiri taarifa kwa haraka bila kufuatilia mfumo ama mbinu yoyote maalum.
Kampuni inasema kuwa vitendo hivyo havinuiwi kuchukua nafasi ya bindamu mbali kusaidia kuimarisha maisha ya wanadamu kwa ujumla.
Kwa mujibu wa wataalamu Darrell M. West na John R. Allen kutoka Taasisi ya Brooklyn nchini Marekani, Akili mwigo ni muhimu katika usalama wa taifa kwani inawezesha Jeshi la Marekani kukusanya taarifa nyingi kwa njia ya video kuhusu usalama na kisha kuzitumia katika kukabiliana na tisho lolote la usalama wa nchi na Wamarekani kwa jumla

Madhara ya akili mwigo

Hata hivyo teknolojia hii inaweza kutumiwa visivyo
Kwa mfano katika uchaguzi wa mwaka wa 2017 nchini Kenya kampuni iliyoungwa ya Cambridge Analytica kutoka Uingereza ilihusika kwa njia kubwa katika kubadilisha taswira ya uchaguzi huo.
Kampuni hiyo ilisemekana kugawanya wakenya kwa kutuma jumbe mtandaoni, kuandika hotuba na hata kubadilisha sura ya chama cha Jubilee kwa njia ambayo ilikifanya kuonekana kuwa bora zaidi na hata kushinda uchaguzi mkuu ambao kisha baadaye uliharamishwa.
Taarifa hizo zilionyesha kuwa viongozi wa upande wa upinzani hawafai ila wale tu wa chama cha Jubilee.
Hata hivyo kuna mengi mazuri kuhusiana na teknolojia ya akili mwigo kama vile kupunguza makosa ya kibinadamu, kuharakisha utenda kazi na kuibua mbinu tofauti za utendaji kazi

admin

One thought on “Akili mwigo, teknolojia inayosoma na kufasiri tabia yako

Leave a Reply

Your email address will not be published.