Acha uchochezi na unyamaze kama hautusaidii, Koome amwambia Mutunga

Acha uchochezi na unyamaze kama hautusaidii, Koome amwambia Mutunga

Shinikizo la Jaji Mkuu Mstaafu Dr. Willy Mutunga kuwataka majaji kugoma kama njia ya kuonyesha kutoridhishwa na hatua ya serikali kukaidi maagizo ya mahakama limepata pingamizi kutoka kwa Jaji Mkuu Martha Koome.

Koome amesema shinikizo hilo linavunja moyo hasa ikizingatiwa kuwa Dr. Mutunga mwenyewe alikataa hatua ya majaji kugoma wakati alipokuwa jaji mkuu.

This image has an empty alt attribute; its file name is Dr-Willy-Mutunga-e1593956236529.jpg
Jaji Mkuu Mstaafu Dr. Willy Mutunga Picha: Kwa Hisani ya MUHURI


Mutunga alikuwa amesema kiwango ambacho serikali inakiuka maagizo ya mahakama cha kuogofya na ni mgomo tu ambao unaweza kuifanya serikali kuamka kutoka lindi la ukaidi na kuanza kutii maagizo hayo.

Wakili Mbishi Miguna MigunaThis image has an empty alt attribute; its file name is download-3.jpg
Wakili Miguna Miguna

Mutunga pia alisema yuko radhi kusafiri hadi nchini Canada kusaidia kumrudisha nyumbani wakili mbishi Miguna Miguna ambaye serikali ilimpiga marufuku kuingia nchini na kisha kutoa ilani kwa kampuni zote za usafiri wa ndege zisiwahi jaribu kumbeba kumleta humu nchini.

Miguna alijipata matatani kwa kumwapisha kinara wa ODM Raila Odinga kama rais wa wananchi jambo ambalo liliikera serikali iliyoanzisha harakati za kumsarisha kwa lazima hadi Canada nchi ambayo ana uraia wa pili.

Hata hivyo alipowasilisha kesi mahakamani alishinda keso zote dhidi ya serikali mna maaisa wake lakini serikali ikakaidi kutekeleza maagizo ya mahakama, jambo ambalo lilielekea kumkera Dr. Mutunga

Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari Jaji Koome anasema kuwa shinikizo la Mutunga ni uchochezi ambao unanuiwa kukwamisha juhudi za wakenya kupata haki hasa ikizingatiwa kuna kesi nyingi mahakamani ambazo zinahitaji kutatuliwa.

Koome anasema kuwa Mutunga alipoapishwa kama Jaji mkuu aliamua kutii sheria na kutunza katiba na hili halijabadilika kwa sababu amestaafu.

Njia mbadala kutatua migogoro


Koome amekariri kuwa kuna njia za rahisi za kutatua migogoro kando na migomo na ambazo Mutunga mwenyewe ashawahi kutumia kusuluhisha shida hizo.

Kwa mfano Rais Kenyatta alipokataa kuteua majaji 11 kati ya 25 walioteuliwa na Tume ya Huduma za Mahakama Jaji Mutunga alitumia mbinu ya majadiliano kutatua mgogoro huo.

Shinikizo la Mutunga limeonekana kama mtihani mkubwa kwa Koome ambaye ni jaji wa tatu mkuu. Majaji wawili waliomtangulia walifanya kazi kwa kutumia uanaharakati mwingi dhidi ya serikali.

Jai Mutunga ni mwanaharakati wa siku nyingi na alifuatiwa na Jaji Maraga ambaye licha ya kuonekana kuwa mdhaifu pale mwanzo aliingia uanaharakati huku akifanya maamuzi na kutoa taarifa ambazo zilionekana kuikera serikali.

Wadadisi wa maswala ya sheria wamesema Koome anakaa vuguvugu na hajaonyesha dalili zozote za kuikabili serikali. Koome kwa upande wake anasema atafuatilia mbinu ya mjadala na diplomasia katika kutatua maswala yanayoikabili idara ya mahakama.

admin

Leave a Reply

Your email address will not be published.